aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, April 3, 2014

WEMA AZUA TIMBWILI GLOBAL, AJIITA YEYE NI CHIZI KULIKO MACHIZI WOOTE!


Stori: Sifael Paul
HOVYOOO! Wema Isaac Sepetu aliye pia Miss Tanzania 2006, amejitoa fahamu kwa kupandisha mzuka na kutinga makao makuu ya Kampuni ya Global Publishers, Bamaga-Mwenge, Dar na kuzua timbwili la aina yake kisa kikiwa ni kuandikwa kwa habari zake na mpenziwe, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Wema akiwa ndani ya ofisi za Global na sura ya 'kuua mtu', mkononi akiwa na gazeti la Ijumaa Wikienda lenye stori: DIAMOND ATAMANI USHOGA. Kushoto ni mpambe na mfanyakazi wake Petit Man Wakuache.
Tukio hilo la kumchoresha staa huyo mwenye vituko kila kukicha, lilijiri Jumatatu iliyopita kwenye ofisi za Global ambao ni wachapishaji wa gazeti hili (Amani), Uwazi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi na Risasi majira ya mchana kweupe hivyo kufunga mtaa huku wapita njia wakimzodoa kwa maneno ya kejeli.
ATINGA NA WAPAMBE DHAIFU
Akiwa na kundi la wapambe dhaifu na goigoi wakiongozwa na meneja wake, Martin Kadinda waliosimama nje ya ofisi hizo, Wema alifika kwa upole akionekana mkarimu kwa mlinzi ambapo aliomba kuonana na mwandishi nguli wa magazeti pendwa, Imelda Mtema.
Mlinzi alimruhusu kwa vile Global ni mjengo wa mastaa na watu wasio mastaa, huwa hawakauki kuingia na kutoka kwa mambo mbalimbali.
Wema alipofika mapokezi, pia aliomba kuonana na mwandishi huyo lakini tofauti na utaratibu ambapo huwa mgeni akifika huulizwa kama ana ‘apointimenti’ ili aitiwe anayemhitaji, Wema alipitiliza kwa nguvu hadi chumba cha habari akifuatana na kijana aliyekuwa akimrekodi.
Wema akiwa ndani ya News Room akimtafuta mwandishi wa Global Imelda Mtema, huku akisema yeye ni chizi!
Akiwa ndani ya chumba cha habari, Wema aliuliza kwa sauti ya juu na ya kujiamini: “Imelda yupo wapi? Nauliza Imelda yupo wapi?”

WEMA NA IMELDA
Katika kumtafuta Imelda kwa macho kwa sababu chumba cha habari ni kikubwa huku akionywa na wahariri kwamba atulize mzuka kisha aeleze shida yake, Wema alimuona Imelda akitoa maelezo kwa Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa ya Global, Oscar Ndauka kuhusu habari aliyokuwa ameifuatilia.
Cha kushangaza, Wema alimfuata Imelda mpaka kwenye meza ya mhariri huyo kisha kuanza kufoka kwa sauti ya juu.
MSIKIENI WENYEWE
“Kwa nini mnafuatilia maisha yangu? Kila siku mnaniandika na Diamond. Kwa nini Imelda unaniandika kuwa mimi msagaji?”
"Mimi ni chizi, nakwambieni mimi ni chizi zaidi ya machizi wote"....Wema alikuwa akifoka mwanamke!
ATULIZWA, AGOMA
Katika kuhoji huko, mhariri kiongozi alijaribu kumtuliza Wema ambaye alikuwa kama amewehuka: ”‘Wema tuelewane, eleza shida yako kwa utaratibu kwani hakuna ofisi isiyokuwa na utaratibu.”
Pamoja na kuambiwa hivyo bado Wema aliyekuwa ameshika Gazeti la Ijumaa Wikienda toleo la Jumatatu iliyopita, aliendelea kumng’ang’ania Imelda ambaye alikuwa akijaribu kumtuliza:
“Wema twende tukakae pale kwenye meza ya mkutano uwaeleze viongozi wangu tatizo lako. Hiyo stori kuwa wewe ni msagaji mbona haipo, ni gazeti gani?”
"Mimi ni chizi, msinitanie ohhh!!
Licha ya kupewa mwongozo huo, Wema aliendelea kufoka:
“Hivi mnajua mimi ni chizi? Kwa taarifa yenu mimi ni chizi zaidi ya machizi wote, ohooo!”

MLINZI ATONYWA, ATIA TIMU
Baada ya hali kuwa tete, mlinzi wa geti kuu alipigiwa simu ya mezani na kujulishwa juu ya Wema kusababisha kazi kusimama ambapo alifika haraka tayari kwa kumtoa nje kwa hiyari yake au lazima.
Ndipo kukatokea timbwili kubwa, wapambe wake ‘goigoi’ nao waliingia wakitaka kufanya vurugu ili kumteka mwandishi huyo lakini kikosi imara cha Global kikiongozwa na Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Championi, Saleh Ally kilijiimarisha na kutuliza fujo hizo huku kikiwa makini kuhakikisha Wema na timu yake hawajeruhiwi hata kidogo.
WEMA ATUMIA GAZETI KAMA SILAHA
Katika purukushani hiyo, Wema alionesha udhaifu wa kumudu varangati pale alipotumia gazeti aliloshika kumpiga nalo mwandishi Imelda, jambo lililodhibitiwa kama Waasi wa M23 wa Kongo walivyodhibitiwa na Majeshi ya Umoja wa Mataifa, akatolewa nje.
Wema akiwa nje ya ofisi sasa baada ya kutolewa kwa nguvu, yeye pamoja na wapambe wake
MBALI NA WEMA
Ukiachia mbali Wema kutulizwa kwa kutolewa nje kwa nguvu, vijana wake walegevu nao waliwekwa chini ya himaya ya Global kwa kunyang’anywa  kamera ya video iliyokuwa ikitumika kuchukua matukio huku nao wakipigwa picha za kutosha na wapiga picha wetu.
VITA KUBWA, WEMA AVUA VIATU
Nje ya ofisi, ‘vita’ kubwa kati ya Wema na walinzi wa Global (alifika mwingine kutoka lindo la mbali) ilizuka ambapo staa huyo alivua vile viatu vyake virefu vya rangi ya bluu bahari na kuanza kumpiga navyo mmoja wa walinzi hao akiamini anamkomesha lakini pia akadhibitiwa!
Wema akiwa ameshika viatu vyake vya mchuchumio mkononi baada ya kutolewa nje ya ofisi na wapambe wake akiwemo meneja wake, Martin Kadinda (kulia).
Wema akiwa anarandaranda kwenye geti kuu akiwa peku, alidondosha matusi ya nguoni ambayo hayaandikiki gazetini kwa namna yalivyokuwa makali. Ilikuwa si rahisi kuamini kuwa yeye ni kioo cha jamii.
Timbwili la Wema na wapambe wake akiwemo Petit Man, ambao hawakufua dafu kwa walinzi na vijana wa Global nje ya ofisi hizo, lilichukua zaidi ya nusu saa huku likikusanya kadamnasi na kusababisha mtaa kujifunga wenyewe.
Wema akiwa kafura ka' faru aliyekoswa koswa kung'olewa kipusa na majangili, kulia ni mpambe na mfanyakazi wake Petit Man Wakuache.
POLISI HAO
Hata hivyo, uongozi wa Global uliwasiliana na Polisi wa Kituo cha Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar ambao walifika na kumkuta Wema na timu yake wakiwa wamepoa mlangoni, wakaambiwa timbwili limetulia hivyo wakatimua zao.
'Baby' wa Diamond Platnumz alikuwa hashikiki viatu viligeuka kuwa 'mzigo mzito' akivibagwa chini huku akitoa mkwara akiwa pekupeku na kufunga mtaa.
Ilibidi askari polisi waitwe kuja kuhakikisha utulivu unakuwepo huku wapita njia wakiwa hawaamini macho yao kuwa wanayemuona mbele yao 'peku peku' akimwaga mitusi ni Miss Tanzania, Wema Isaac Sepetu!
APEWA KAMERA, KADI NOOOO!
Baadaye Wema aliomba kupewa kamera yake ambapo zoezi hilo lilifanyika lakini ‘memori kadi’ yenye picha walizoanza kurekodi, ilitolewa ili kupisha maridhiano kwanza. Waliambiwa kadi hiyo ilitolewa kwa sababu walirekodi bila idhini au kibali cha Kampuni ya Global.
Miongoni mwa watu waliokuwa kwenye msafara wa Wema ni pamoja na Ammy Nando (kushoto), mshiriki wa Big Brother Africa 'The Chase' ya mwaka jana ambaye alikuwa akificha sura kukwepa kamera za Global.
WEMA AGOMA KUONDOKA
Baada ya kugundua kadi ya kamera ipo chini ya ulinzi wa Global, Wema alitaka kulianzisha tena akidai hawezi kuondoka hadi apewe kadi hiyo lakini uongozi uliweka ngumu. Baadaye aliondoka kimyakimya. Wakati huo wapambe wake walishaondoka kitambo.
WEMA: CHIZI in action......
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, kadi ya kamera hiyo bado ilikuwa inashikiliwa na uongozi wa Global ili kumthibitishia Wema kuwa hawezi kufanya umafia wowote dhidi ya waandishi wa kampuni hiyo yenye nguvu kihabari nchini Tanzania.
Gari lake lililomleta Global kufanya timbwili.
KWA NINI?
Kwa mujibu wa Wema, magazeti ya Global yamekuwa yakimwandika vibaya yeye na mpenzi wake Diamond huku akitolea mfano wa habari iliyomhusu yeye na mwigizaji Aunt Ezekiel baada ya kunaswa kwa picha zao zilizoashiria vitendo vya usagaji.
source:gpl

No comments:

Post a Comment