aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, April 9, 2014

LADY JAYDEE APATA SHAVU LA KUFA MTU.. ASHIRIKI KWENYE WIMBO WA KOMBE LA DUNIA 2014...

 
Msanii mkongwe wa muziki nchini Judith Mbimbo maarufu kama Lady Jaydee ameshiriki kuimba wimbo maalum wa kombe la dunia 2014 akishirikiana na David Correy na rapper wa Kenya, Octopizzo ...
  
Katika wimbo huo, Lady Jaydee na Correy wameimba kwa lugha yaKiingereza huku Octopizzo ‘akichana’ kwa Kiswahili.
 

Wimbo huo ulipigwa kwa mara ya kwanza wiki hii jijini Dar es Salaam wakati kampuni ya Coca-Cola ilipozindua promosheni yake mpya ya miezi miwili ya Kombe la FIFA la Dunia 2014 ambayo itawawezesha wateja wake kujishindia zawadi mbalimbali zikiwamo tiketi za kwenda kushuhudia mechi za robo fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil.