aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, April 23, 2014

ANGALIA PICHA KIBAKA APIGWA MPAKA KUPOTEZA MAISHA KWA TUHUZA ZA WIZI HUKO CHUO CHA MZUMBE

kibaka akiwa amevaa vazi la single batani huku ameshikilia vifurushi vya viatu na nguo alizodaiwa kuiba

 Kijana Mmoja aliyetuhumiwa kuwa Kibaka Akiwa amesimama kwa Huruma mara baada ya Kushushiwa Kipigo na wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe cha Morogoro ..Kibaka huyo akiwa amelala chini mara baada ya Kupigwa

Tukio hilo lilitokea wiki iliyopita saa nane na nusu usiku huku mvua ikinyesha ambapo kibaka huyo anayeishi nje ya Chuo hicho alikamatwa na wananchi wakazi wa karibu na chuo hicho akiwa na kifurushi cha viatu na nguo akiwa amevaa vazi la single batani  ndipo walipomuhoji mahala alipoiba na kusema ameiba chuoni na ndipo wananchi hao waliamua kumpeleka chuoni hapo kwa kipigo kikali ambapo tukio hili lilidhihirisha ujirani mwema wa wanakijiji waishio pembezoni mwa chuo hicho na wanafunzi wa chuo cha mzumbe ambapo walipofika chuoni hapo katika moja ya hosteli wanaoishi wanaume ijulikanayo kama kibasira wakamwongezea zaidi kipigo na ndipo wanafunzi nao wakaamka na kufanya yao na kumuadhibu barabara.. kwani kwa habari tulizozipata kutoka kwa shuhuda chuoni hapa inasemekana wizi umekithiri sana kwani wanafunzi wamekuwa wakiibiwa laptop na nguo chuoni hapa ambapo inasemekana hosteli moja ijulikanayo kama nyirenda kwa kipindi cha mwezi mmoja na nusu ziliibiwa laptop 8 huku tano zikiwa zimeibwa kwa mkupuo (kwa siku moja) sasa wakawa kama wanakumbushwa machungu hayo..

mida ilipozidi kuyoyoma hali isiyo ya kawaida mpaka inafika saa kumi kasoro hapakuwa na mlinzi wa aina yeyote aliyewasili katika tukio hilo kumnusuru maisha ya kibaka huyo richa ya kupiga kelele akidai anakufa na huku akiomba maji ya kunywa na kuamsha wanafunzi wengi huku pakiwa na makelele ya hapa na pale  na ndipo mwanafunzi mmoja baada ya kumuonea huruma mwizi huyo akaamua kumpigia simu waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi wa chuoni hapa hali ya kustaajabisha zaidi waziri huyo alijibu kuwa hawezi kuamka kwani amelala.. na ndipo kijana huyo alipoamua kumpigia simu waziri wa ulinzi na ndipo alipofika na walinzi wawili wa chuoni hapo na kukuta wazee wa kazi(wanafunzi) wakiendelea kumsurubu kwa bakora za matako kibaka huyo maeneo ya shule ya msingi mzembe ambapo kibaka huyo alikuwa tiari hajitambui na ndipo walipomchukua na kuondoka nae majira ya saa kumi alfajiri.....!