aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, April 24, 2014

MAPICHA YA POMBE SIO SUPU:ALEWA CHAKARI, ALALA STENDI

Vitabu vya Mungu vinataja kila kitu ni lazima kiwe na kiasi, ukizidisha basi kinachoweza kutokea ni aibu. 

Jamaa mmoja ambaye jina halikupatikana mara moja, alijikuta akipata aibu ya mwaka baada ya kunywa pombe na kulewa chakari na
Katika hali ya sintofahamu kijana mmoja amekutwa akiwa amelewa chakali na kulala kwenye stendi ya mwenge.
kukata ‘netiweki’ jambo lililosababisha ‘aangushe gari’ pembeni mwa stendi ya daladala ya Mwenge jijini Dar.
Ishu hiyo ilitokea wiki iliyopita ambapo paparazi wetu alibahatika kushuhudia laivu jamaa akijigeuzageuza kama yuko kitandani kwake.Kufuatia tukio hilo, kibaka mmoja aliamua kumgeuza dili mlevi huyo kwa kumsachi na kumchania mifuko yote ya suruali jamboWananchi wakifanya jitihada za kumuamsha.
lililowaudhi waliokuwepo jirani na kumng’ang’ania mwizi huyo kutaka kumshushia kichapo.
“Samahani, msinifanye kitu chochote  sitarudia tena, nimefanya kosa sana, naomba mnisamehe ndugu zangu,’’ kibaka huyo alijitetea.

“Ushukuru Mungu tunakufahamu wewe, ila hujafanya kitendo cha kiungwana kabisa, unaweza kufa unajiona hivihivi, wewe si una 
Akiwa hajiwezi kutokana na ulevi uliokithili.
nguvu?  Kwanini usifanye kazi kama wengine?’’ alihoji mmoja wa  watu waliotaka kumpiga kibaka huyo.
Mwandishi wetu aliamua kutafuta njia mbadala ya kumsaidia jamaa huyo wa gambe kwa kushirikiana na wasamaria wema ndipo maji 

ya baridi yalipochukua nafasi kama huduma ya kwanza kwa kummwagia mwili mzima.
Baada ya kumwagiwa maji jamaa huyo alipata nguvu akaamka  na kuanza kuangaza macho huku na huko.

Hakuishia kufanya hivyo tu, aliinuka na kuanza kuondoka kwa kujikongoja lakini alipigwa butwaa baada ya kubaini mifuko yake yote ilichanwa kwa wembe.
Jamaa huyo alipoulizwa alikuwa akiishi eneo gani alijibu Ubungo, akapandishwa kwenye daladala iliyokuwa ikielekea huko.

No comments:

Post a Comment