aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Tuesday, April 29, 2014

WATOTO WA NGURUMO WAANZA KUTOANA ROHO YARABI HATA KABLA YA 40 KUFIKA..


“Tunatoana roho yarabiii, kwa mali alizoacha baba…” hicho ni kibwagizo katika wimbo wa Tunatoana Roho uliopigwa na Msondo Music Band ukiwa ni utunzi wa marehemu TX Moshi William akishirikiana na marehemu Muhidin ‘Maalim’ Gurumo na waimbaji wengine wa bendi hiyo!
Nyumba ya marehemu mzee Gurumo.
Yawezekana Gurumo alikuwa akijitabiria kitakachotokea baada ya kifo chake kwani kabla hata arobaini ya kifo chake ikiwa bado haijatimia, songombingo la aina yake limezuka katika familia yake baada ya watoto kudaiwa kuanza kuzigombea mali alizoziacha baba yao.
GARI ALILOPEWA NA DIAMOND
Utata umeanzia katika gari aina ya Toyota FunCargo alilopewa zawadi na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ ambapo inadaiwa kuwa mtoto mmoja wa marehemu (jina tunalo), ameshajitangazia kuwa ni lake.
Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ akimkabidhi funguo ya gari aina ya Toyota FunCargo mzee Gurumo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho ni ndugu wa karibu wa familia hiyo, siku moja baada ya msiba, mtoto huyo alitangaza kuwa gari hilo ni lake na akaanza kutafuta madalali wa kuliuza gari hilo lakini akakwamishwa na kukosekana kwa kadi ya gari.
“Yaani hawa watoto wa marehemu sijui wana nini jamani, hata arobaini ya baba yao bado wameanza kushikana mashati, hii ni hatari sana. Huyo mmoja ndiyo anajitapa kabisa kuwa gari ni la kwake na ameshaanza kutafuta mteja,” kilisema chanzo chetu kwa masharti ya kutotajwa gazetini.
DALALI WA NYUMBA ANATAFUTWA
Yote tisa, kumi ni nyumba aliyokuwa anaishi marehemu na familia yake, iliyopo Makuburi, Ubungo. Kwa mujibu wa chanzo chetu, nyumba hiyo tayari ipo sokoni na madalali wanahaha huku na kule kusaka wateja ili iuzwe.
“Mjane wa marehemu anatia sana huruma. Unajua bado yupo kwenye eda, hata arobaini ya mumewe haijafika watoto wameanza kumchachamalia wanataka kuuza hata nyumba anayoishi, sasa ataenda wapi? Tunaomba nyie waandishi wa habari mumsaidie huyu mama, watamdhulumu kila kitu,” kilisema chanzo.
Mke wa marehemu mzee Gurumo, Pili Nassoro.
UWAZI KAZINI
Baada ya kupata taarifa hizo, Uwazi liliamua kuingia mzigoni ili kuupata ukweli wa madai hayo mazito.
MSIKIE MTOTO WA MAREHEMU
Uwazi lilimtafuta mtoto wa marehemu, Mariam Gurumo ambaye alipoulizwa kuhusu ishu hiyo, alisema:
“Aliyekupa hizo taarifa ni muongo, hakuna ishu kama hiyo. Kwanza bado tunaomboleza kifo cha baba yetu. Sasa tuuze gari na nyumba ili iweje? Siyo kweli.
“Ni kweli kuna kesi ya nyumba ipo mahakamani lakini siyo nyumba hiyo unayoisema. Unajua sisi watoto wa Gurumo tunataka kudhulumiwa nyumba iliyoachwa na marehemu mama yetu iliyopo Ilala.
“Unajua huyu mjane wa marehemu, hakubahatika kupata mtoto, sisi mama yetu ni marehemu na tulizaliwa wanne, mimi (Mariam), Mwalimu, Mwazani na Omary.
“Abdallah yeye ana mama mwingine lakini ni ndugu yetu wa damu. Kabla mama hajafa, Gurumo alimjengea nyumba Ilala.
“Sasa mama yetu alipokufa, mdogo wake (jina tunalihifadhi) akawa anataka kuiuza, hivi jana tu (Ijumaa) tumetoka mahakamani. Tumefungua kesi pale yenye jalada namba RB/IL/112/2013 kuzuia nyumba kuuzwa. Tunashukuru mahakama imeingilia kati vinginevyo tungedhulumiwa.
Naomba watu wasichanganye, nyumba yenye matatizo ni ya Ilala. Kuhusu gari, kwa sasa bado hatujaamua chochote mpaka arobaini ipite,” alisema Mariam.
HUYU HAPA MJANE WA MAREHEMU
Uwazi halikuishia hapo, lilienda mpaka nyumbani kwa marehemu  nakuzungumza na mjane wa marehemu, Pili Nassoro ambaye alifunguka mazito. Hebu msikie:
Binti wa marehemu mzee Gurumo, Mariam Gurumo.
“Ni kweli nyumba inauzwa. Hilo lilikuwa ni agizo la mume wangu kabla hajafariki, aliniambia ni bora aiuze kabla hajafa kwani anawajua wanaye watanisumbua sana pindi akifa.
“Tulianza kutafuta wateja miezi minne kabla Gurumo hajafa, bahati mbaya ametangulia kabla hatujakamilisha hiyo kazi. Yeye alikuwa na lengo zuri la kutaka atugawie kila mmoja chake ili akifa yasitokee haya yanayotaka kutokea.
“Unajua hii nyumba tumejenga na mume wangu, mimi nilikuwa mfanyabiashara na tulisaidiana kabla hata hawa watoto hawajazaliwa lakini nashangaa wanataka kunigeuka eti mimi sihusiki.”

MJANE AILILIA SERIKALI IMSAIDIE
“Naomba serikali iingilie kati kwenye hili suala, nyumba wala gari viziuzwe kwanza. Jamani hata eda sijamaliza mambo yameanza kuwa hivi.
Hao watoto wenyewe tangu tumzike baba yao hawajakanyaga hata hapa nyumbani kunijulia hali, sijui wanafikiria nini kuhusu mimi, naomba mnisaidie nimalize eda salama na mali zikiuzwa, basi na mimi nipewe staahili yangu,” alisema mjane huyo kwa huzuni.