MOHAMMED IQBAL DAR.
Nimeona niwafahamishe hili huenda likatusaidia hasa kwa hivi sasa wakati tukisherekea miaka 50 Muungano, najua wengi wetu hatujui historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar maana tuliwakuta waasisi wetu wameishafanya zoezi hilo , tusilijadili sana kwa kuwa lengo lao lilikuwa zuri.
Lakini je unamjua huyu Bwana aliyetunga jina la Tanzania pata historia ya namnaalivyofanikiwa kupata jina la T A N Z A N I A.
Sherehe za Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar huwa tunasherekea kila Mwaka Tarehe 26/04/ lakini Tangu mimi binafsi nipate ufahamu na kuanza kushuhudia sherehe za Muungano nimekuwa nikisikia kuwa jina la Tanzania lilipendekezwa na Watanganyika, Wazanzibar na Raia wengine wa nje lakini sikuwahi kukutana na huyo ambae alibuni jina hili tamu la Tanzania.
Imekuwa kama Bahati nimekutana na Mtu huyu aliyebuni jina la Tanzania Mkoani Mtwara.
Huyu bwana aliyebuni jina la Tanzania ni Muhindi na Dini yake ni AHMADIYA MUSLIM JAMAAT TANZANIA majina yake ni MOHAMMED IQBAL DAR.
Mohammed alizaliwa Mkoani Tanga miaka ya 1944, Baba mzazi wa Mohammed alikuwa Daktari huko mkoani Morogoro alikuwa anaitwa Dr. T A DAR alikuwa Tanganyika kuanzia mwaka 1930.
Mohammed Iqbal Dar alipata elimu yake ya Msingi Mkoani Morogoro shule ya Msingi H H D AGHAKHAN kwa sasa ni Shule ya Serikali na baada ya hapo alikuja baadae kujiunga Mzumbe akasoma Kidato cha Kwanza mpaka cha Sita, na baadaye
na Chuo cha mzumbe.
Aliingiaje kwenye shindano la kupendekeza jina la Muungano kati Tanganyika na Zanzibar ?
Mohammed anasema alikuwa Maktaba akijisoma gazeti la Tanganyika Standard, siku hizi Daily News, akaona Tangazo linasema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unafahamika kama Republic of Tanganyika and Zanzibar jina likaonekana refu sana kwa hiyo Wananchi wote wakaombwa Washiriki kwenye shindano la Kupendekeza jina moja litakalo zitaja nchi zote mbili yaani Tanganyika na Zanzibar Mohammed Iqbal Dar anasema aliamua kuingia kwenye Shindano na hivi ndivyo alianza Safari ya Kubuni Jina la Muungano.
Kwanza anasema alichukua karatasi akaandika Bismillah Raahman Rahimu hii ni kutokana na Imani yake na baada ya hapo akaandika jina la Tanganyika baada ya hapo akaandika Zanzibar halafu akaandika jina lake Iqbal halafu akaandika jina la Jumuiya yake ya Ahmadiya baada ya Hapo akamrudia tena Mwenyezi Mungu akamwomba amsaidie ili apate jina zuri kutoka katika majina hayo aliyokuwa ameyaandika. Baada ya hapo Mohammed Iqbal Dar alichukua herufi tatu kutoka Tanganyika yaani TAN na kwa upande wa Zanzibar akachukua Herufi tatu za Mwanzo ZAN ukiunganisha unapataTANZAN alivyoona hivyo akachukua I herufi ya kwanza katika jina lake la Iqbal na akachukua A kutoka jina la dini yake yaani Ahmadiyya kwa maana hiyo ukiongeza herufi hizi mbili I na A kwenye TANZAN unapata jina kamili TANZANIA akalisoma jina akaliona ni zuri lakini akajiridhisha pia kwamba akiongeza herufi hizo za I na A kwenye TANZAN italeta maana kwakuwa nchi nyingi za Afrika zinaishia na IA, mfano EthiopIA, ZambIA ,NigerIA, TunisIA, SomalIA, GambIA, NamibIA, LiberIA, MauritanIA alivyoona hivyo akaamua apendekeze kuwa jina TANZANIA ndio litumike kuwakilisha nnchi hizi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar kwa maana hiyo jina TANZANIA limezaliwa kutoka majina manne majina hayo ni Tanganyika, Zanzibar, Iqbal na Ahmadiyya.
Mohammed Iqbal Dar baada ya kupata jina hilo akalituma jina hilo kwenye kamati ya kuratibu Shindano. Baada ya Muda mwingi kupita baba yake na Mohammed Iqbal Dar alipokea barua nzito kutoka Serikalini ikiwa inasomeka kama ifuatavyo…
REPRESENTED BY THE
MINISTRY OF INFORMATION AND TOURISM , TANZANIA
TO
MOHAMED IQBAL DAR
IN RECOGNATION OF THE ACHIEVEMENT OF CHOOSING THE NEW NAME FOR THE
UNITED REPUBLIC OF TANGANYIKA AND ZANZIBAR
“ REPUBLIC OF TANZANIA ”
DURING THE NATIONAL COMPETITION DAY IN 19TH NOVEMBER 1964
I A WAKAL
MINISTER FOR INFORMATION AND TOURISM
Barua hiyo pia ilisema...
Utakumbuka kuwa miezi michache iliyopita ulituandikia kutupa ushauri kuhusu jina jipya la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na wewe pamoja na wananchi wenzio 16 ulishauri nnchi yetu iitwe Tanzania . Nafurahi kukuarifu kuwa mshirikiane ile Zawadi ya sh. 200 iliyoahidiwa na leo nakuletea check ya sh. 12/50 ikiwa ni hisa yako katika zile sh.200. Nashukuru sana kwa jitihada ya kufikiri jina la Jamuhuri yetu.
Barua ikasainiwa na Idrisa Abdul Wakil Waziri wa Habari na utalii kipindi hicho.
Sasa kwa nini Mohamedi Iqbal Dar anadai yeye kuwa mshindi pekee wakati barua ilikuwa inaonyesha kulikuwa na washindi wengine 15 ambao nao walishinda?
Jibu ni kuwa wakati wa kutolewa kwa Zawadi hizo hakuna aliyejitokeza zaidi ya Bwana Mohammed Iqbal Dar na Bwana Yusufal Pir Mohamed ambaye hata hivyo alikosa sifa baada ya kushindwa kutoa barua ya kumpongeza kuwa ameshinda kwa madai kuwa Barua ameipoteza, hivyo Wizara ya Habari na Utalii iliamua kumtangaza bwana Mohammed Iqbal Dar kuwa Mshindi na kumpatia zawadi yote ya sh.200/; pamoja na Ngao.
Bwana Mohammedi Iqbal Dar anasema anachosikitika ni kuwa mchango wake bado Watanzania hawathamini mchango wake lakini yeye anaipenda Tanzania na anajivunia kuwa Mtanzania japo anadhani dini yake ya Uislamu ndiyo tatizo hawataki kutambua mchango wake ila anaamini kuwa siku moja ukweli utajulikana.
Hayo ni maelezo ya Mohammed Iqbal Dar ambaye kwa sasa anaishi Uingereza kwa kuwa huko ndiko alipata kazi eneo la Birmigham b35 6ps UK , Dar– es-Salaam House, 18 TURNHOUSE ROAD , PHONE 44 121-747-9822
Nimeona niwatumie hii wadau wangu ili tuweze kuongeza ufahamu na kama ulikuwa unalijua hili basi nimekukumbusha pia mambo yalivyokuwa miaka ya 1964.
No comments:
Post a Comment