aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, April 30, 2014

PRODYUZA MANECKY NA MADAI YA KUZAA NA RIYAMA,

NYUMA ya mafanikio ya wasanii wa muziki kuna  wengi wanachangia lakini mara nyingi ni kama hawajulikani. 
Prodyuza mkali Bongo kutoka AM Records, Emmanuel Saimon Sewando ‘Manecky’.
Hata wakijulikana,sifa huenda moja kwa moja kwa msanii tu.Maprodyuza wana mchango mkubwa sana, maana wakitengeneza ngoma mbaya, mwisho wake ni kwamba msanii hawezi kutoka.

 Leo hapa
kwenye Exclusive Interview tunaye Prodyuza mkali Bongo kutoka AM Records, Emmanuel Saimon Sewando ‘Manecky’.
Je, unajua kuwa nyimbo kibao za wasanii kama Diamond, Suma Lee, Ali Kiba, Keisha na wengineo zina mkono wake?
Manecky amefafanua mengi juu ya kazi zake za muziki, maisha binafsi na skendo kadhaa zinazotajwa dhidi yake.
Msanii wa filamu Riyama Ally
INADAIWA DIAMOND HATAKI KUFANYA KAZI TENA NA WEWE KWA SABABU ULIACHIA WIMBO WAKE WA NATAKA KULEWA BILA RIDHAA YAKE, IMEKAAJE?
Ujue wasanii wana mchezo ukimaliza kazi yake, anaomba demo na kuiweka kwenye simu yake, sasa wana katabia ka kuachia
chinichini (kwa kuwarushia rafiki zao kwa simu) ili kusikiliza wadau wanavyopokea.
Ikipokelewa vizuri, anaitoa au akiona ina upungufu fulani anaifanyia mabadiliko haraka, ndicho kilichotokea kwa Diamond.
Mimi nisingeweza kuachia singo yake bila idhini yake.
Kwanza ili iweje? Halafu singo yenyewe iliyoachiwa ilikuwa haina hata lebo yangu, sasa ingekuwa na faida gani na mimi? Sijambo la kweli.
INAELEZWA UNA UHUSIANO WA KIMAPENZI NA MSANII WA FILAMU, RIYAMA ALLY NA UMEZAA NAYE. FAFANUA.
Hapana. Riyama ana maisha yake, ana mwenzake na mtoto wake.
Kilichopo ni kwamba nipo naye karibu kikazi, halafu kwa bahati mbaya, jamaa yake na Riyama anafanana sana na mimi, nadhani watu wanashindwa kututofautisha.
LAKINI INASEMEKANA RIYAMA ALIKUPORA MIKONONI MWA ROSE NDAUKA NA UHUSIANO WAO SASA SI MZURI, KISA NI WEWE. UNASEMAJE?
Siyo kweli. Hata hivyo, sipendi kumzungumzia Rose kwa sababu ana mtu wake na kila mtu anajua. Siyo vizuri kusema chochote
kilichotokea kati yangu na yeye wakati uliopita.
UNAKUTANA NA CHANGAMOTO GANI KWENYE ‘GAME’?
‘Sometimes’ wasanii hawataki kubadilika, unaweza ukamshauri abadilishe baadhi ya vitu kwenye wimbo wake ili uwe wa tofauti
anakataa. Tatizo wanakariri.
Mfano; nakumbuka wakati natoa idea yangu kuboresha wimbo wa Hakunaga wa Suma Lee, hakunielewa. Ilifikia mahali
tukakorofishana studio, lakini mimi nilikuwa natetea kitu kizuri.
Ona sasa, mwisho wa siku, ngoma imetoka imekuwa mzuka. Jamaa amepiga shoo nyingi sana. Ni kwa sababu alitoa kitu cha tofauti.
Sasa hivi wasanii kibao wanamuiga.
TAJA TOP 6 YAKO YA WASANII WA BONGO FLEVA
Wa kwanza kabisa ni Lady Jaydee, huyu mdada ni mkali. Ameanza zamani na mpaka sasa hajachuja. Anajua muziki, amewekeza kwenye
biashara na anajua anachokifanya.
Wengine ni Ben Pol, Vanessa Mdee, Diamond, Ali Kiba na AY. Hawa nawakubali sana. Wapo kwenye nafasi za juu kwa upande wangu.
KUNA MADAI KUWA WASANII WA KIKE WANA SHINDWA KUWIKA KWA SABABU WAKIJA STUDIO MNAWATAKA KIMAPENZI, IMEKAAJE HIYO?
(Anacheka sana) Kama wapo walio kwamishwa kwa mtindo huo nadhani wamejitakia wenyewe tu. Hivi msanii kama amekuja kikazi,
utaweza kujiingiza kwenye mambo ya kimapenzi?
Utakuta msanii anakwenda studio, amevaa kimitego halafu usiku! Unategemea nini? Hata sisi ni binadamu bana (anacheka tena).