aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, April 17, 2014

JE WAJUA HARUSI YA RAY NITAKUWA MWANDAAJI CHAKULA ASEMA JOHARI

MKONGWE kwenye sanaa Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amefunguka kuwa endapo ikitokea mkurugenzi mwenzake, Vincent Kigos akaoa, yeye atajitolea kuwa mwandaaji wa chakula.
Mkongwe kwenye sanaa Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’.
Akizungumza na mwanahabari wetu mwishoni mwa wiki iliyopita, Johari alisema yeye na Ray ni watu wa karibu kwa kuwa wameiongoza kampuni yao kwa muda mrefu hivyo katika jambo muhimu kama la ndoa, lazima ajitoe kinaga ubaga kufanikisha.
Msanii wa Bongo Muvi, Vincent Kigosi 'Ray'.
“Yani hata kama ikitokea kesho mkasikia Ray anaoa ujue kabisa nitakuwa muandazi kuhakikisha madikodiko yanawafikia waalikwa kwa wakati muafaka,” alisema Johari ambaye mara zote amekuwa akikanusha kuwa uhusiano wa kimapenzi na Ray.

CREDIT - GPL