aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, April 26, 2014

SNURA ALIWATAKA WANAUME WAKWARE WAACHE KUMSUMBUA KWA SABABU AMEMPATA MWANAUME SAHIHI MAISHANI MWAKE

STAA wa wimbo wa Majanga, Snura Mushi anaonekana kugandwa na mahaba niue baada ya hivi karibuni kuanika hisia zake na kuonesha dhahiri kuwa amezama vilivyo kwenye penzi motomoto la jamaa yake aitwaye Hunter Sleiyum.  
Staa wa wimbo wa Majanga, Snura Mushi akiwa kwenye mahaba mazito na boyfriend wake aitwaye Hunter Sleiyum.
Snura aliwataka wanaume wakwale waache kumsumbua kwa sababu amempata mwanaume sahihi maishani mwake, anafurahia mapenzi na uzuri zaidi mpenzi wake anampenda yeye pamoja na mwanaye.
Snura Mushi akiwa na Hunter Sleiyum.
“Hata kuamua kufanya kazi hii ya kunengua majukwaani ni kwa sababu nilikwepa mambo ya kujiuza kwa wanaume, kazi hiyo siiwezi kabisa, niko tofauti na wengine wanaokubali kujiuza na kutothamini miili yao,” alisema Snura.

Mbali na kumzungumzia mpenzi wake huyo ambaye ni DJ wa Maisha Club, Snura alikanusha kuhusu taarifa za kutajwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mchezaji wa Yanga, Mrisho Ngasa.

“Huwezi kuamini, Ngasa hajawahi kutoka na mimi, alikuwa ni mshkaji tu,” alisema Snura.