aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, April 26, 2014

MTOTO WA KAJALA AUMIZWA NA UGOMVI WA MAMA YAKE NA WEMA "NAMPENDA SANA WEMA"


Kutokana na ugomvi unaoendelea kati ya Wema Sepetu na Kajala Masanja,mtoto wa Kajala aitwaye Paulette amesema anaumizwa na ugomvi huo na kwamba amekuwa akimtumia ujumbe Wema kumweleza anavyompenda. 

Paulette alikuwa akizungumza na ‘Movie Leo’ ya kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM.
 

“Vimekuwa vinaniuma sana ila hata kama wakisema vitu vyote ataendelea kuwa mama yangu,” alisema. 

“Mimi naona mama yangu hana makosa yoyote wanavyomtukana,mimi nakuaga najisikia sana vibaya.

"Namwambia (Wema) mama yangu hata kama amekosea kitu chochote amsamehe kwasababu mimi nampenda Wema kama aunt yangu na ninampenda mama yangu tena sipendi nikiona wanatukanana wala nini napenda wawe marafiki,nataka nimwambie Wema nampenda sana,” alisema. Paula.