aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, April 26, 2014

AUNTY LULU ACHEZEA KICHAPO KUTOKA KWA MPENZI WAKE BAADA YA KUTAKA KWENDA KLABU USIKU BILA KUMTAARIFU.

MSANII wa filamu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ hivi karibuni alijikuta akichezea kichapo kutoka kwa mpenzi wake anayejulikana kwa jina la Amani baada ya kutaka kwenda klabu usiku bila kumtaarifu.
Msanii wa filamu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ akipozi.
Kwa mujibu wa majirani, tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo walimsikia msanii huyo akipiga mayowe na walipotoka walimuona akipigwa.
“Kwa kweli alipigwa sana na sasa amevimba uso,” alidai mmoja wa majirani aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Paparazi wetu alimtafuta Aunty Lulu lakini hawakuweza kuonana naye kwani aligoma akidai kwa hali aliyonayo hawezi kuonana na waandishi ila akasema:
“Ni kweli Amani kanipiga, kaniumiza ila siwezi kuliongelea sana suala hilo, haya ni mambo yetu binafsi.”