aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, May 31, 2014

INAKUWAJE MDADA MZURI KAMA HUYU ANAWEKA PICHA HIZI KWENYE MTANDAO WA INSTAGRAM..PAPARAZI AZIFUMANIA





TUNALAANI VIKALI VITENDO HIVI....... INSTAGRAM WAFUNGIENI WAPUUZI HAWA!!!

MAKUBWA..!! KIJANA ANAEDAIWA KUWA NI MSUKULE,AONEKANA NJE YA NYUMBA YA KIKONGWE ALIYEUAWA KWA USHIRIKINA,NI SIKU MOJA BAADA YA MAZISHI YA KIKONGWE HUYO

Kijana Ndaki Samola akiwa amepandishwa ndani ya gari la
polisi kwa ajili ya kupelekwa kwa wataalamu ili kufanyiwa
uchunguzi kama ana matatizo ya akili.

 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mamia ya wananchi wa kijiji cha Ilebelebe kata ya Itilima wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wamefurika kushuhudia tukio la kijana mmoja anayesadikiwa kuwa ni msukule aliyeibuka siku moja baada ya kikongwe kuuawa kwa kucharangwa mapanga kwa imani za kishrikina kijijini hapo. 
 
Kijana huyo aliyedai kuwa anaitwa Ndaki Samola alionekana jirani na nyumba ya mwanamke Nyanzala Basu (65-70) aliyeuawa Mei 26 mwaka huu,saa moja na nusu usiku baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana kisha kumcharanga mapanga akiwa nyumbani kwake kisha kutokomea kusikojulikana. 
 
Imeelezwa kuwa siku ya mazishi ya Kikongwe huyo Mei 27 mwaka huu ndipo kijana huyo anayedaiwa kuhifadhiwa na kikongwe huyo alikutwa na wananchi nyuma ya nyumba ya kikongwe huyo saa tatu usiku akizunguka na kusikika akisema kaamua kutoka nje baada ya kukosa chakula. 
 
Walioshuhudia tukio hilo walisema Kijana Ndaki Samola anayedaiwa kuwa ni msukule akizungumza kwa shida alisema anatoka kijiji cha Bubale kata ya Samuye wilaya ya Shinyanga na alifika kijijini hapo kwa ajili ya kuoa. 
 
Kijana huyo akizungumza bila ya kufafanua ni kipindi gani amekaa katika kijiji hicho alidai alikuwa akiishi kwenye nyumba ya bati ya kikongwe huyo na wenzake wawili na kwamba kutokana na njaa yake ndiyo kaamua kutoka. 
 
Mwenyekiti wa kijiji cha Ilebelebe Thomas Nkindo alisema tukio hilo limewashangaza kwani kijana huyo hajawahi kuonekana kijijini hapo hata siku moja ,hali ambayo imewapa wasiwasi wananchi kutokana na maneno aliyoeleza kwamba alikuwa kwenye nyumba ya kikongwe huyo ambayo ilikuwa imefungwa kwa muda mrefu na haitumiki. 
 
“Baada ya kuhojiwa na jeshi la jadi sungusungu kijana, alidai kilichomtoa ndani ni njaa na kawaacha wenzake wawili mmoja akiwa ni mwanamke,na alikuja kwa ajili ya kuoa na kufikishiwa kwenye nyumba hiyo ya tope ambayo imeezekwa kwa bati iliyokuwa ikimilikiwa na marehemu”,alieeleza Nkindo. 
 
Akifafanua zaidi kuhusu tukio hilo afisa mtendaji wa kijiji cha Ilebelebe Emmanuel Asili alisema marehemu Nyanzala Basu kabla ya kufikwa na mauti siku hiyo ya tukio asubuhi alikuwa amealika wanawake, ambao walifanya kazi ya kumsaidia kukata viazi maarufu kama michembe ndipo usiku huo huo alivamiwa na kuuawa majira ya saa 1.30 wakati akimpatia mbwa wake chakula. 
 
 
“Kilichotushtua zaidi huyo kijana Ndaki alikuwa ananukia harufu ya nyama wakati tunamuona na ukizingatia mchana kwenye mji huo ulipokuwa msiba walikuwa wamechinja mbuzi,moja kwa moja wananchi walimtilia mashaka inawezekana akawa ni msukule kwa kulinganisha na maelezo yake “alisema Asili. 
 
“Kutokana na mashaka hayo tulitoa taarifa kwa jeshi la polisi huku tukimhifadhi kijana kwa muda katika ofisi yangu uangalizi zaidi na polisi walipofika walizungumza na wananchi na kuamuru mlango wa nyumba hiyo uvunjwe ili kuona kilichomo ndani wakakuta beseni,ndoo na bati lililochakaa”,alieeleza afisa mtendaji wa kijiji. 
 
Akizungumza na wananchi mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya Kishapu ASP Samwel Kijenga aliwataka kutoa ushirikiano ili kuwabaini watu waliosababisha mauaji hayo ya kinyama huku akiwataka kuondoa wasiwasi kuhusu nyumba waliyokuwa wakihofia kwani wameangalia hawajaona kitu hivyo waendelee na shughuli za maendeleo. 
 
Hata hivyo wakati kijana huyo akiwa tayari amepandishwa ndani ya gari la polisi kwa ajili ya kupelekwa kufanyiwa uchunguzi kama ana matatizo ya akili,alitokea mwanamme aliyejitambulisha kwa jina la Nyalali Chaba mkazi wa kijiji cha Ikoma wilayani Kishapu na kudai kuwa anamfahamu ni mdogo wake anasumbuliwa na tatizo la akili ndipo polisi wakamkabidhi kwa maandishi. 
 
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga SACP Evarist Mangalla amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la mauaji ya kikongwe na tayari watu wanne wanashikiliwa kwa ajili ya mahojiano zaidi wakati wakiendelea na upelelezi

TUMEFANIKIWA KUZIPATA PICHA ENZI ZA UHAI WAKE ZA MWANAFUNZI ALIYEFARIKI LEO MCHANA KATIKA HOSTEL ZA CHUO KIKUU MLIMANI (UDSM)

ENZI ZA UHAI WAKE....


 







source:paparazi

KUMRADHI PICHA ZINATISHA SANA: DEREVA BODABODA AUAWA KIKATILI NA MAJAMBAZI KWA KUCHINJWA SHINGO...FUNGUA HAPA.

ANGALIA PICHA ZA MAREHEMU GEORGE TYSON MASAA 4 KABLA YA KIFO CHAKE PAMOJA NA GARI ALILOPATA NALO AJALI.

IMG_4162
Marehemu Geogre Tyson pichani hapa alikuwa yupo kijiji cha Chilonwa Chamwino kwenye utoaji wa madawati katika shule ya msingi Chaula iliyopo Dodoma.

 Baada ya kumaliza shughuli hii huku akiwa kama producer wa The Mboni Show mauti yalimkuta majira ya saa 12 jioni masaa 4 tu toka tuanze safari ya kurudi Dar es Salaam maeneo fulani hivi kama unataka kukaribia GAIRO mjini.
Katika gari hilo walikuwa watu 8 ila yeye pekee ndio aliyepoteza maisha na wengine kupata majiraha mwilini pamoja na dereva wa gari hilo. Kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa Morogoro katika  hospital ya mkoa Morogoro, baadae asubuhi mwili utaanza safari ya kuelekea Dar es Salaam.
IMG_4166IMG_4176 IMG_4213IMG_4214IMG_4215
Kweli ajuae mwisho wetu ni Mungu pekee. Tunaishi kama vile tunajua maisha yetu yataisha lini kumbe tunajidanganya. Haya matukio yote ni kwa ajili yetu kuamka na kujifunza kitu. Tumrudieni Mungu, tuungame dhambi zetu maana hakuna ajuae siku wala saa yake itakuwa lini. R.I.P Tyson na wote mliotutangulia.

MC ZIPOMPA NAYE ANUSURIKA AJALI ILIYOMUUA TYSON!..WALIKUWA WAMEPANDA GARI MOJA

MC maarufu Gladys Chiduo maarufu kwa jina la MC Zipopamba (pichani) amenusirika kifo baada ya gari kupata ajali na kumuua George Tyson. Zipompa ameuambia mtadao huu asubuhi hii kuwa yeye alikuwa kiti cha mbele na Tyson pamoja 

watu wengine walikuwa viti vya nyuma na kilichomuokoa yeye ni kufunga mkanda, kwani licha gari kupinduka na kuzunguruka mara tatu alipata majeraha kidogo na hali yake inaendelea vyema kwa sasa akiwa hospitali ya Mkoa ya Morogoro. 

JOHARI AMTUPIA CHUCHU VIJEMBE MSIBANI

STAA wa Bongowood, Blandina Chagula ‘Johari’ anadaiwa kumtupia vijembe kiaina msanii mwenzake, Chuchu Hans ambaye ‘anabanjuka kimalovee’ na mkurugenzi mwenza wa Kampuni ya RJ, Vincent Kigosi ‘Ray The Greatest’. 
Staa wa Bongowood, Blandina Chagula ‘Johari’.
Tukio hilo lilichukua nafasi kwenye msiba wa mwigizaji Sheila Haule ‘Recho’ Sinza-Palestina, Dar, hivi karibuni ambapo vijembe viliibuka baada Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Nyerere’ kumuuliza kwa lugha ya utani Chuchu kuwa RJ itachangia nini msibani hapo, Johari akadakia:
“Kampuni yangu si ya uchochoroni au ya chumbani, nina TIN namba kabisa siyo kama hiyo nyingine, iweje umuulize asiyehusika...”
Baada ya Johari kutamka maneno hayo, waombolezaji waliokuwepo msibani hapo walipigwa na butwaa na kuhoji kulikoni?
Mastaa wa Bongo Muvi akiwemo Chuchu Hans (wa pili kushoto) wakiwa msibani kwa Recho.
Johari amekuwa akidaiwa kuwa na uhusiano na Ray kipindi cha nyuma huku kukiwa na taarifa kuwa Chuchu ana kampuni iitwayo Chura ikimaanisha Chuchu na Ray hivyo ilitafsiriwa kuwa alikuwa akiipiga kijembe kwa madai kuwa haiwezi kufikia levo za RJ.
Alipofuatwa na paparazi ili kupata ufafanuzi juu ya ishu hiyo, Johari hakuwa tayari kwani alisema ana majonzi ya kuondokewa na kipenzi chake Recho hivyo hakutaka malumbano na watu katika kipindi hiki kigumu.

Friday, May 30, 2014

SABABU 5 ZINAZOKUFANYA UOE AU KUOLEWA NA MTU AMBAE SI CHAGUO SAHIHI KATIKA MAISHA YAKO


KUNA baadhi ya sababu zinazosababisha watu kuoana pasipo kufanya 

maamuzi sahihi. Wanandoa wengi huingia katika ndoa wakitegemea mambo 
mengi kubadilika, kitu ambacho ni makosa yanayosababisha ndoa nyingi 
kuvunjika.Kabla ya kuoa/kuolewa unapaswaUjitambue Kwanzana ujiulize 
maswali kadhaa, kwanza jiulize;(1)Je huu ni wakati sahihi?(2)Kwa 
ninimtu huyu? na(3)Unamuoa au kuolewa na mtu atakaye kuwa sambamba na 
malengo yako katika maisha yako yote?Wakati kuna sababu kadhaa za 
kumuoa/kuolewa na mtu sahihi, pia upande mwingine kuna sababu kibao 
zinazopelekea watu kuoa watu wasio sahihi kwao. Kabla ya kusema 
"Ndiyo" zingatia sababu tano hapa chini zinazokufanya uoe au kuolewa 
na mtu ambaye si sahihiambae baadae hupelekea kutengana na kupeana 
taraka.(1) Tumekuwa katika mahusiano kwa muda mrefu. Kuwa katika 
mahusiano kwa kipindi kirefu sio sababu pekee ya kufanikiwa kumpata 
mwenye mafanikio katika maisha yako, unaweza ukawa umemvumilia kwa 
muda mrefu na sasa ukaamua tu kwasababu umekwisha zoea tabia yake na 
kufuata usemi wa"maji ukisha yavulia nguo shartiuyaoge".(2)Msukumo wa 
Marafiki- Rafiki zangu wote wamekwisha OA/KUOLEWA....... itabidi na 
mimi nioe/niolewe. Kufuata mkumbo wa makundi katika jamii sii kitu 
kizuri, kwani ndoa siyokitu cha kubeep na kuacha. Jipange kwanza na 
muda ukifika basi itaingia katika ndoa yenye mpangilio mzuri wa 
maisha.(3) Sidhani kama nitaweza.Usipo jiamini na kujipenda mwenyewe 
sidhani kama itakuwa rahisi kumpenda mtu mwingine unayetegemea kuwa 
nae maishani.(4) Mategemeo ya kuboresha tabia ya mwenza wako. Tukisha 
oana nitambadilisha tabia. Cheti cha ndoa siyo leseni ya kumrazimisha 
mwenzi wako kubadilika kwa lazima. Jaribu kuwa na subira na kumtafuta 
mwenzi mnae endana nae kitabia.(5)PESA- Anakazi nzuri naamini ataleta 
pesa au anatoka katika familia ya kitajiri. Kunaukweli mkubwa katika 
misemo ya wahengayani "kama ukiowa kwaajili ya pesa, basi utazilipa" 
japokuwa kuwa na pesa sio vibaya, lakini hii haitazuia pia haizuii 
kuwa na muunganiko mbaya wa ndoa.Wanandoa wengi huingia katika dimbwi 
hili ambapo wengine hushinikizwa kuoa kulingana na taratibu za kimila 
au kidini. Lakini pia wazazi wakati mwingine huchangia ndoa nyingi 
kuvunjika, ikiwa ni kwa kuwachagulia wananandoa mke au mume.Vijana 
ambao bado hamjaoa au kuolewa"Jitambueni Kwanza", fikirini kwa kina 
kabla ya kufanya maamuzi yasiyo sahihi ambayo yatawagharimu muda wenu 
na kupata mateso ya muda mrefu.

KUFANYA MAPENZI OFISINI HUVURUGA SAIKOLOJIA YA MTU.

Kula nanasi kunahitaji nafasi, wengi wamekuwa wakishawishika 
kufanyamapenzi katika eneo la kazi kutokana na kupendana ama 
vishawishi mbali mbali kutoka kwa kinadada hususani katika mavazi. 
Sina maana mbaya ninaposema kina dada kwasababu wengi wao ndio 
wanaoacha sehemu zao nyeti wazi, kwamfano kuvaa nguo fupi sana na 
kuvaa vitop vinavyoonyesha sehemu kubwa ya maziwa wazi.Kwa asilimia 
miamoja watu wengi wanaofanya mapenzi kwa kuiba katika maeneo kama ya 
ofisini huwahawakumbuki kuvaa kinga kutokanana mihemumko mikali na ya 
haraka kuliko kawaida wanayokuwa nayo kwa wakati huo. Ni vyema 
kujihadhali ma mihemuko hii kwani madhara yake ni makubwa.Mihemuko hii 
huwakumba watu wote hata ambao wako katika ndoa, kutokana na 
vishawishi vya mwenzake basi anajikuta amezama katika saa za kazi. 
Tabia hii ikifanyika mara tatu huanza kuwa kama sehemu ya majukumu ya 
wezihawa wa mapenzi. Kinadada wanaovaa nguo fupi katika makazi ya watu 
huenda wakawa wanafanya hivyo kwasababu ya fasheni, wengine kutafuta 
mvuto kwa wafanyakazi wenzie, lakini kwa wanaume huwa ni kishawishi 
kimoja kikubwa sana.Kumbuka unapaswa kuishinda faragha yako na 
kujitambua kuwa hupaswi kufanya mapenzi na mke wa mtu au mume wa mtu. 
Unapoona vishawishi kama hivi jaribu kuwa bize na kazi, chukulia poa 
tu japokuwa wadada wengi huwa na njia mbali mbali za kukufanya ukanasa 
kirahisi kwa mfano kama mnakumbuka skendo ya Monica Lewinsky na 
aliyekuwa rais wa Marekani wakati huo walichokifanya ofisini na baadae 
kuja kuwa ni skendo kubwa sana.Hasara ya mapenzi hayo ya kiwizi wizi 
katika masaa ya kazi ni kupata maambukizi ya Ukimwi bila kufahamu 
kwani utakuwa umemzoea mfanyakazi mwenzio kwa jinsi alivyo smati 
katika kazi, hivyo hutafikilia kama anawatu wengine nje ya kazi. Pia 
kuna maambukizi ya magonjwa ya zinaa, ambayo kwa wanawake hujificha 
kwa muda kabla ya kuonekana haraka kama wanaume.

MADHARA YA KUFANYA MAPENZI KUPITA KIASI


Katika hali ya kawaida kufanya mapenzi kuna faida nyingi, lakini 
linapokuja suala la kuzidi kiasi tunapata matatizo ya msingi ambayo 
huleta madhara kwa watu wanaoendekeza sana ngono.Kuna watu ambao 
hawezi kulala bilakufanya mapenzi na huku wengine wakikosa uwezo wa 
kuvumilia hata kwa siku mbili au tatu.Mtu anaweza kuwa na mke na 
kujikuta kila siku anatumia 'chakula cha usiku' kwa sababu tu hakuna 
wa kumkataza na kwamba ana haki ya kufanya hivyo kwa sababu amelipa 
mahari.Hilo linaweza kuwa jambo jema kwaupande mwingine, lakini 
uchunguzi unaonyesha kuwa watu wengi kati ya watu wanaolalamika 
kupoteza hisia za kimapenzi hutoka katika kundi la watu wapenda 
ngono.Pamoja na tatizo hilo, yapo madharamengine mengi ambayo mtu 
asiyekuwa na kiasi katika tendo la ndoa anaweza kukabiliana nayo, 
hivyo ni vema tukajifunza ili tusiwe watu wa kuendekeza miili kiasi 
cha kulazimika kufanya mapenzi kila tunapokutana hata kwenye nguzo ya 
umeme na chini ya miti kwa vile tu miili imetaka kufurahika.Twende 
pamoja katika kutazama madhara hayo kwa kina.KUPOTEZA HAMU YA 
TENDO.Watu wenye pupa za kufanya mapenzi hupoteza haraka hisia za 
kimapenzi kwa wapenzi wao kutokana na sababu za kisaikolojia 
zinazoweza kujitokeza wakati wa ufanyaji wa tendo la ndoa mara kwa 
mara.Sababu hizo zinaweza kuwa ni pamoja na zile za kumzoea 
mwenzakiasi cha kukosa msisimko hata anapomuona akiwa mtupu.Aidha 
kukinai haraka staili za kimapenzi kunatajwa kujitokeza kutokana na 
kukutana mara kwa mara kwa aina zile zile za mapenzi na pengine sehemu 
moja, kitanda kimoja na chumba kile kile, jambo ambalo linaweza 
kumfanya mhusika asione jipya kutoka kwa mwenza wake na hivyo kupoteza 
hamu naye na kuhisi kama hawezi tena kushiriki tendo la ndoa 
kikamilifu.KUUJAZA MWILI TAMAA KUBWA.Tabia ya kufanya mapenzi mara 
kwamara huongeza uzalishaji wa homoni mwilini na kuufanya mwili uwe na 
msukumo mkubwa wa kutaka kuridhishwa kwa tendo la ndoa bila kukosa na 
hivyo kumfanyamhusika asiwe mtu mwenye uwezo wa kuzuia tamaa na kukosa 
chaguo la nani wa kufanya naye mapenzi nakwa wakati gani?Watu 
wanaojiendekeza katika kufanya mapenzi mara kwa mara ndiyo wale ambao 
kila wanayemtazama barabarani humtamani bila kujali hadhi yake.Hawa 
ndiyo wanaobaka, kusaliti ndoa zao hata kwa watumishi wa ndani au 
kufanya mapenzi na watoto wao wa kuwazaa kwa vile akili zao huwa 
zimeathirika kwa tamaa ya mapenzi.Unapokuwa mtu wa kufanya mapenzi 
mara kwa mara huwezi kuwa na uwezo wa kuzuia tamaa yako. Mumeo 
akiondoka siku mbili unatamani kuwa hata na houseboy ili akukate kiu 
ya penzi.KUPOTEZA RAHA KAMILI YA TENDO.Raha ya tendo hutegemea sana 
hisia iliyokuzwa kutokana na mapenzi sahihi na kiu ya kufanya mapenzi, 
hivyo basi ukiwa mtu wa kufanya mapenzi kila mara unawezakupoteza 
msisimko wa tendo na kujikuta unapata furaha ambayo haikutoshi 
kumaliza tamaa yako.Kama ni mapenzi utakuwa unayafanya kwa mazoea tu 
na msisimko wako utakuwa mdogo!KUPOTEZA NGUVU ZA MWILI.Madhara mengine 
yanayoweza kupatikana kwa kufanya mapenzi mara kwa mara ni pamoja na 
kupoteza nguvu nyingi za mwili.Kama tujuavyo tendo la ndoa hasa kwa 
wanaume huwafanya watumie nguvu nyingi, hivyo kuufanya mwili uchoke. 
Aidha lishe inapokuwa ndogo kwa wafanya mapenzi mwili hukosa nguvu za 
kutosha kuhimili misukosuko ya kimaisha.Sambamba na hilo mbegu za 
uzazi zinazotoka kwa wanaume wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa 
dhaifu.KUPATA MAGONJWA.Kama tulivyojifunza kuwa watu wanaofanya 
mapenzi mara kwa mara huwa na tamaa na hujikuta wanafanya mapenzi 
holela ambayo huweza kuwasababishia magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi, 
lakini ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na msukumo wa kutosha hasa kwa 
wanawake huwafanya waishiwe msisimko na kuzifanya sehemu zao za siri 
kutotoa ute unaoweza kuwakinga na michubuko wakati wakujamiiana na 
hivyo kuwasababishia michubuko itakayoweza kuleta maambukizi ya haraka 
ya magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi.

NGUO ZINAZOFAA KUVALIWA CHUMBANI UKIWA NA MPENZI WAKO


mumewe hata kama amechoka au ana 
hasira kwa siku hiyo...Ndugu yangu uchawi 
rahisi kwa mumeo ni kumvalia nguo 
nyepesi na yenye kuonyesha maumbile 
yako kamili,hii inaweza kuwa gauni nyepesi 
inayoonyesha maumbile yako ama siku hizi 
kuna mitandio milaini ambayo pia unaweza 
kuivaa pindi unapokuwa na mwenzi 
wako,ikumbukwe pia wanaume wengi 
hupatwa na tatizo la ukosefu wa nguvu za 
kiume kwa kukosa hisia za kufanya tendo 
hilo lakini wanawake ni dawa nzuri ya 
tatizo hilo ikiwa ataweza kumuhamasisha 
mumewe kwa njia mbalimbali ikiwemo ya 
vazi ambalo litamfanya mzee asisimke.. 
Mapenzi ni hisia,na hisia hizo huwa kwa 
wote yaani kwa wanaume pamoja na 
wanawake,baadhi ya walio kwenye 
uhusiano huwalalamikia sana wenzi wao 
na sababu kuu huwa ni kutokuwa na hamu 
ya kufanya nao tendo la ndoa.Hapa 
nitazungumzia mavazi yanayopaswa 
kuvaliwa chumbani hasa mnapokuwa 
wawili tu yaani mke na mume.. 
Mwanaume siku zote huwa na hisia za 
haraka sana hasa ukimjulia,lakini baadhi ya 
wanawake huwa wanashindwa kuzijua 
haraka mbinu za kumpandisha mzuka 
mumewe hata kama amechoka au ana 
hasira kwa siku hiyo...Ndugu yangu uchawi 
rahisi kwa mumeo ni kumvalia nguo 
nyepesi na yenye kuonyesha maumbile 
yako kamili,hii inaweza kuwa gauni nyepesi 
inayoonyesha maumbile yako 
ama siku hizi kuna mitandio milaini ambayo 
pia unaweza kuivaa pindi unapokuwa na 
mwenzi wako,ikumbukwe pia wanaume 
wengi hupatwa na tatizo la ukosefu wa 
nguvu za kiume kwa kukosa hisia za 
kufanya tendo hilo lakini wanawake ni 
dawa nzuri ya tatizo hilo ikiwa ataweza 
kumuhamasisha mumewe kwa njia 
mbalimbali ikiwemo ya vazi ambalo 
litamfanya mzee asisimke