aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Tuesday, April 1, 2014

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI:KIJANA AUWAWA LEO ASUBUHI KWA KUCHOMWA MOTO AKITUHUMIWA KUIBA PIKIPIKI ILEMELA MWENZAKE ANUSURIKA

 
Mtu mmoja anaesadikiwa kuwa ni jambazi ambaye hakufahamika  jina anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 25 ameuwawa kwa kupigwa mawe kisha kuchomwa moto na mwingine kunusurika kuuwawa.

Tukio hilo limetokea alfajiri ya leo katika kijiji cha Shibula kata ya Bugongwa wilayani Ilemela Mkoani Mwanza kufuatia tukio la wizi lilotokea usiku wa kuamkia leo katika mtaa Nyamwilolelwa ambapo pikipiki moja na paneli ya solar ziliibiwa.

Katibu wa Sungusungu katika kijiji cha Shibula John Mashalia amesema kuwa kufuatia tukio hilo  waliamua kuweka ulinzi shirikishi kuzunguka vijiji vyote na ndipo walipokutana na kijana huyo aliyeuwawa akiwa na kijana mwingine aliyefahamika kwa jina la Edward Aloyce ambao walidai wanatafuta pikipiki iliyopotea.

Mashalia ameongeza kuwa kata ya Bugongwa imekuwa na matukio ya ujambazi mara kwa mara ikiwa ni pamoja na vitendo vya ubakaji kwa watoto na wanawake.

Kwa upande wake mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi Joyce Kotecha amewataka wananchi wa kata hiyo kuacha kujichulia sheria mkononi na kwamba wawasiliane na uongozi wa kata yanapotokea matatizo ya namna hiyo.