aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, April 4, 2014

AFRIKA KUSINI YAANZA KUGAWA BURE KONDOM ZENYE RANGI NA HARUFU NZURI KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI

 
Serikali ya Afrika Kusini imeanza mpango wa kuwapa bure vijana wa shule za sekondari kondom zenye rangi tofauti tofauti na ambazo zina harufu nzuri ya kuvutia. 
 
Mpango huu unalenga kuzuia wanafunzi kuchoka kutumia mipira ya kawaida ya kondom wanaposhiriki ngono. Waziri wa afya Aaron Motsoaledi, ameyasema hayo baada ya utafiti uliofanywa nchini humo kuonyesha kuwa matumizi ya mipira ya kondom imepungua nchini Afrika Kusini. Inaarifiwa kinachosababisha upungufu huo ni kwamba kondom za kawaida zinazotolewa na serikali hazina mvuto wowote kwa vijana.
 
Afrika Kusini ina watu milioni 6.4 wanaoishi na virusi vya HIV, idadi hiyo ikiwa juu zaidi kuliko nchi yoyote duniani. Utafiti uliofanywa na kitengo cha serikali cha utafiti wa afya, ulionyesha maambukizi yameongezeka hadi asilimia 12.2. Takriban watu milioni 2 hupata matibabu ya ARV’s au madawa ya kupunguza makali ya HIV.
 
Hata hivyo baadhi ya mashirika ya misadaa yanaonya kuwa baadhi ya kliniki zinakabiliwa na upungufu wa dawa hizo.


Source:BBC

No comments:

Post a Comment