aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, March 6, 2014

TAIFA STARS WAWATOA JASHO NAMIBIA KWAO, WAKITOKA SARE YA 1 - 1

TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania Taifa Stars leo imetoka sare ya kufungana bao 1-1 na Namibia katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa Sam Nujoma nchini Namibia.clip_image001Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa sbila ya nyavu za timu yoyote kuguswa huku kipindi cha pili kilikuwa kipindi cha ingia toka nyingi kwa Stars kwani walifanya mabadiliko ya hapa na pale,
Dakika ya 30 ya kipindi cha pili Stars ilifanya mabadiliko kwa kutoka Erasto Nyoni na Juma Luizio na kuingia Michael Pius na Mcha Khamis
Ilipoingia dakika ya 85 Stars baada ya kuona mambo bado mazito wakafanya mabadiliko mengine akatoka Ramadhan Singano na kuingia Athanas Mdamu.
Taifa stars ndio walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 86 kupitia kwa Khamisi Mcha 'Viali' kwa mpira wa kona aliopiga na kuingia moja kwa moja mpaka kwenye nyavu za Namibia bila kuguswa.
Namibia walisawazisha bao hilo katika dakika ya tano ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za kawaida, lililofungwa na Nekundi Haleluya Panduleni kwa adhabu, na kupelekea mchezo kwisha kwa sare ya goli 1-1.