aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, March 13, 2014

ANGALIA PICHA ANUSURIKA KUFA BAADA YA KUCHOMWA NA KITU CHENYE NCHA KALI KICHWANI:

clip_image001
Liu Fenghe akiwa hospitali na chuma kichwani.
clip_image001[6]Picha ya X-ray ikionyesha jinsi chuma hicho kilivyoingia kichwani mwa bwana Liu.

FUNDI majengo Liu Fenghe wa nchini China, amenusurika kifo baada ya kuchomwa na chuma kichwani na kuzama inchi 8 ambazo ni sawa na sentimita 20.
Liu alikuwa akiongea na rafiki yake na kwa bahati mbaya alidondokewa na chuma hicho kilichomchoma kichwani.
Rafiki yake Liu aitwaye Zhang anasema:

"Ilikuwa ghafla. Kabla sijafanya chochote Liu alikuwa katika dimbwi la damu."Inadhaniwa kuwa chuma hicho kilidondoka kutoka ghorofa ya 25 ya jengo walilokuwemo mafundi hao mpaka kusababisha maafa hayo.
Madaktari walimfanyia upasuaji wa haraka katika hospitali iliyopo jimbo la Shanghe nchini China na kueleza kuwa Liu hayupo tena katika hatari japo bado haijajulikana ni lini ataweza kurudi kazini.