aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, March 26, 2014

MLINZI WA BARACK OBAMA AMEACHISHWA KAZI KWA KOSA LA KULEWA CHAKARI KAZINI.

obJarida la Washington Post nchini Marekani limeripoti kwamba  askari watatu wameachishwa kazi kwa muda na kurudishwa nyumbani ili uchunguzi ufanyike. 
Askari mmoja kati ya hao ambao wanaohusika na kumlinda rais Barack Obama alikutwa amelewa pombe chakari kwenye hoteli moja huko Amsterdam ambapo Obama alienda huko kwa ajili ya mkutano wa mambo ya Nuclear.
Msemaji wa idara ya upelelezi Marekani alikataa kutoa taarifa zaidi kuhusu tukio hilo ingawa alisisitiza kuwa watatu hao wameachishwa kazi kwa muda uchunguzi ukiendelea.
Mwaka 2013 majasusi wawili waliondolewa katika kikosi cha ulinzi cha Rais Obama kufuatia tuhuma za kuhusika na kashfa ya ngono na utovu wa nidhamu.
Mwaka 2012 majasusi kadhaa waliachishwa kazi kufuatia madai kuwa walikodi makahaba walipokuwa mjini Cartagena Colombia.