UKISIKIA simulizi ya Hafsa Ramadhani (19) itakutia simanzi, itakutesa moyo na kukutoa machozi, huwezi kuamini aliingia kwenye ndoa bila kujua kuwa alikuwa akienda kukutana na ugonjwa wa ukimwi.
Habari kutoka chanzo chetu cha kuaminika zinasema, binti huyo alifanyiwa mipango ya ndoa bila yeye na mumewe huyo kupima kwanza maambukizi ya ugonjwa huo, ingawa tahadhari hiyo ilitolewa mapema kwa kuwa muoaji alikuwa akijulikana kuwa aliishi na ugonjwa huo kwa muda mrefu.
ILIKUWAJE?
“Huyo binti alitokea Bukoba, akaja hapa Dar es Salaam kutafuta kazi. Akaanza kufanya kazi za ndani, akiwa mdogo kabisa. Alihangaika kwenye nyumba mbalimbali lakini baadaye akafikia kwenye kituo cha watoto yatima (kwa sasa tunahifadhi jina), kipo Charambe ambapo alianza kuishi hapo,” kilipasha chanzo chetu kwa sharti la kutotajwa jina lake .
“Alipofikisha umri wa miaka 15 tu, wale watu wa pale kituoni wakamuozesha kwa jamaa mmoja (jina tunalo) ambaye kwa sasa ni marehemu. Huyo jamaa alikuwa akiishi na VVU na mbaya zaidi, hao watu wa hapo kituoni, walishauriwa kuhusu jambo hilo wakapuuza, ndiyo maana wengi wanaamini walimfanyia makusudi,” kilieleza chanzo hicho ambacho kimedai kipo karibu na binti huyo.
HUYU HAPA HAFSA
Timu ya wanahabari kwa msaada wa chanzo chetu, ilifanikiwa kukutana na Hafsa ambaye kwa mwonekano ni binti mdogo na mpole kiasili, akazungumza mengi yanayomsibu katika maisha yake.
“Sikujua kama maisha yangu yangeishia hivi. Sikutegemea kama ningeteseka kiasi hiki. Kwanza mimi sijawahi kuwaona wazazi wangu. Niliambiwa tu walikufa tangu nikiwa mdogo, kwa hiyo nilikulia kwa wazazi wa kufikia huko Bukoba,” anaanza kusimulia Hafsa.
Akaendelea: “Baada ya kuolewa, maisha yalikuwa ya shida sana. Nilichukuliwa hapa Dar na kwenda kuishi na huyo mume wangu Arusha baada ya kufunga naye ndoa. Alikuwa haniachii fedha ya matumizi wakati mwingine lakini hali yake ya kuugua kila mara iliniogopesha ingawa sikuwahi kufikiria kabisa suala la ukimwi.
“Nilibahatika kupata mtoto na huyo bwana na hapo ukawa mwanzo wa mimi kuanza kuugua mfululizo. Nikiwa bado naumwa, mume wangu alifariki dunia. Basi, maisha yangu yakazidi kuwa magumu maana sikuwa na msaada wowote.”
DOKTA AMWAMBIA UKWELI
“Nikiwa nakwenda kliniki huku afya yangu ikiwa si ya kuridhisha, daktari mmoja alinishauri nifanyiwe vipimo. Ilibidi nishauriwe sana kabla ya kupimwa na kwa bahati mbaya nikagundulika kuwa nina ukimwi. Hata mwanangu pia ameathirika.
“Najua walinificha kwa muda mrefu kutokana na umri wangu, maana sasa nina miaka 19 na mwanangu mitatu, kwa hiyo wakati najifungua nilikuwa na 16 tu. Naiona dunia chungu kwa kweli.”
MAISHA MAGUMU ARUSHA, ARUDI DAR
“Kutokana na maisha ya mateso ya ndugu wa mume wangu kule Arusha, nilijikusanya nikapata nauli, nikaamua kutoroka na kurudi zangu Dar. Sikuwa na mahali pengine pa kwenda zaidi ya kurudi kituoni nilipokuwa nalelewa.”
ANYANG’ANYWA MWANAYE
“Mwanangu ndiye alikuwa faraja yangu pekee lakini wakwe zangu walikuja kuninyang’anya mtoto wakisema eti sina uwezo wa kumlea. Kwa kuwa ni damu yao, sikuwa na jinsi ikabidi nikubali tu. Sasa hivi anaishi nao huko Temeke.
“Nashukuru Mungu, nilipata msamaria (aliomba asitajwe jina lake) ambaye aliguswa na ugumu wa maisha yangu, akanikaribisha nyumbani kwake. Naishi naye Mbagala – Zakheem (Dar), lakini nina ugumu wa maisha. Kama unavyojua, siwezi kumtegemea yeye kwa kila kitu.”
ANAHITAJI MSAADA WAKO
Kama umeguswa na kisa cha Hafsa na ungependa kumsaidia kwa hali na mali, unaweza kufanya hivyo kwa kutumia namba 0783 855453 au 0713522779.

No comments:
Post a Comment