aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, March 26, 2014

PICHA ZAONYESHA MABAKI YA NDEGE YA MALAYSIA ILIYOPOTEA BAHARINI

Waziri wa Ulinzi wa Malaysia ambaye pia ni  Kaimu waziri wa Usafirishaji, Hishammuddin Hussein akionyesha picha zinazodaiwa kuwa mabaki ya ndege iliyopotea.

Picha ya Satelite ikionyesha kinachodhaniwa kuwa mabaki ya MH370.
Serikali ya Malaysia imesema kuwa picha mpya za Satelite zimeonyesha zaidi ya vifaa miamoja vinavyodhaniwa kuwa mabaki ya ndege yake iliyotoweka zaidi ya wiki mbili zilizopita.
 Waziri wa usafiri wa nchi hiyo, Hishammuddin Hussein, amesema kuwa picha hizo zilizotolewa na Ufaransa, zinaonyesha vifaa hivyo kuwa zaidi ya mita ishirini kwa urefu.
 Hadi kufikia sasa, hakuna taarifa rasmi ya mabaki ya ndege hiyo kuonekana.
 Ndege hiyo iliyokuwa na abiria 239, ilikuwa safarini kutoka Kuala Lumpur kuelekea Beijing zaidi ya wiki mbili zilizopita.
 Msako uliofanywa baharini na angani, kuitafuta ndege hiyo umeanza tena katika pwani ya Australia baada mawimbi kutulia baharini.


CHANZO: BBC SWAHILI NA DAILYMAIL.

No comments:

Post a Comment