aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Monday, March 31, 2014

HAYA NI MAPATO YALIYOPATIKANA KWENYE MECHI YA SIMBA NA AZAM.

pesaaMechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Azam na Simba iliyochezwa jana Machi 30 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam imeingiza jumla ya sh. 26,455,000,amabyo ilikua na Watazamaji 4,741 walikata tiketi kushuhudia pambano hilo ambapo Azam iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000,mgawanyo kwa mapato ulikuwa kama ifuatavyo Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 4,035,508.47,gharama za kuchapa tiketi sh. 3,908,686 wakati kila klabu ilipata sh. 5,460,687.63,uwanja sh. 2,776,620.83,gharama za mechi sh. 1,665,972.50, Bodi ya Ligi sh. 1,665,972.50.
Mapato mengine yalienda kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 832,986.25 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 647,878.19.

credit:millardayo

No comments:

Post a Comment