aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, March 21, 2014

BAADA YA DOGO JANJA KUTANGAZA MAAMUZI,HII HAPA KAULI YA BABA YAKE MZAZI

Screen Shot 2014-03-21 at 12.53.22 PM

Alhamisi ya March 20 2014 lilitoka tamko ambalo lina maamuzi ya msanii wa bongofleva Dogo Janja kuhusu kuomba msamaha na kuhitaji kurudi kwenye kundi lake za zamani la Tiptop connection na kuyasahau yaliyopita kati yake na aliyekuwa meneja wake pia ambae ni Madee.

baba mzazi wa Dogo Janja amepata nafasi kuzungumza kwa mara ya kwanza baada ya mtoto wake kuomba msamaha.

Anasema >>’Dogo Janja alishakua mtu mzima na tayari nilishawahi kumwambia achague mahali atakapoona kuna manufaa kwake, akishafanya maamuzi yake huwa ananishirikisha kwenye kujadiliana, tayari alishawahi kuniambia kuwa atafanya maamuzi baada ya kuona Mtanashati hakuna muelekeo wowote na hakuna anachopata ndipo akaniambia baba mimi mtu yoyote au kundi lolote nitakalokubaliana nalo basi nitafanya nao kazi’.

Hayo ni maelezo ya Baba mzazi wa Dogo Janja ambae ametoa baraka zote kwa Janja kurudi kujiunga na Tiptop Connection hivyo kazi imebaki kusikia kutoka upande wa Tiptop kufahamu kama wameukubali msamaha wa Dogo Janja.