aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, March 29, 2014

MAKUBWA NA MAZITO HAYA....MAMA SHARO MILIONEA AMVAA KITALE KWA TUHUMA NZITO NA ZA AIBU...!

Mama yake na marehemu Hussein Mkieti  aka ‘Sharo Milionea’ .Makubwa! Mama mzazi wa aliyekuwa nyota wa filamu na muziki, marehemu Hussein Mkieti ‘Sharo Milionea’ amemtuhumu msanii wa vichekesho ambaye alikuwa rafiki wa mwanaye, Musa Kitale kuwa alikula michango ya kumbukumbu ya kifo cha mwanaye, mwaka jana. 
Kwa mujibu wa chanzo makini, Mama Sharo amekuwa akimlalamikia Kitale kwa watu kwamba alikula fedha za mchango wa mwanaye hivyo kupigwa marufuku kwamba kitu chochote kinachomhusu Sharo asipewe.


Ilidaiwa kwamba, chanzo cha mama Sharo kutaka Kitale asipewe kitu chochote kinachomhusu marehemu ni baada ya hivi karibuni Klabu ya Bongo Movie Unity kutangaza kuwa litatoa Tuzo kwa Sharo Milionea kama kumbukumbu kwani alikuwa ni mwenzao katika tasnia ya filamu.
Ilisemekana kuwa mama huyo alielezwa kwamba tuzo hiyo itapokelewa na Kitale ndipo alipokataa na kusema hataki kabisa kitu chochote kipitie kwa msanii huyo kwa sababu huwa hamfikishii. 

 
Msanii wa vichekesho Musa Kitale.
“Mama Sharo amekuwa akilalamika kwa muda mrefu sana kwamba Kitale anatumia vitu vya mwanaye, eti alichangisha michango ya kumbukumbu hakumfikishia hivyo kwa sasa ameamua kupiga marufuku asikabidhiwe kitu chochote,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kupata habari hizo, wanahabari wetu walimtafuta Kitale ambapo kabla hata ya kujibu tuhuma hizo, alinyanyua simu na kumpigia mama Sharo kumuuliza kama kweli amezungumza madai hayo.
Mama Sharo alikiri kuwa ni kweli alizungumza akidai alifikia uamuzi huo baada ya kutonywa na watu kuwa Kitale amekuwa ‘akichikichia’ fedha za marehemu mwanaye.
Kitale, baada ya kujiridhisha, alitoa ufafanuzi kuwa madai hayo hayana ukweli na kudadavua kwamba wakati wa kumbukumbu ya Sharo mwaka mmoja (Novemba) tangu alipofariki dunia, hakuna michango yoyote iliyotolewa.
“Inaniuma sana kwa sababu enzi za uhai wa Sharo hatukuwahi kugombana hata siku moja na mama Sharo alikuwa analitambua hilo, tuliishi kama ndugu na mimi ndiye niliyemsaidia mpaka akapata umaarufu lakini sasa namshangaa huyu mama kunishutumu vitu vya uongo,” alisema Kitale kwa huzuni huku jasho likimtiririka.

No comments:

Post a Comment