aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, March 12, 2014

KIM KARDASHIAN ANUSURIKA KIFO, APATA AJALI YA GARI

clip_image001WAKATI akiwa katika maandalizi ya harusi yake mwanamitindo ambaye pia ni mchumba wa msanii wa Hip Hop nchini Marekani Kim Kardashian jana alipata  ajali ya gari ambayo haikuwa na madhara makubwa wakati akiendesha gari lake aina ya Mercedes G Wagon na kukwaruzana na Nissan Sentra.
Hata hivyo, gari la Kim Kardashian halikuharibika zaidi mkwaruzo mdogo iliupata lakini Nissan Sentra inadaiwa kuharibika vibaya sehemu ya mbele.
Shuhuda wa tukio hilo ameiambia TMZ kuwa Kim Kardashian alikuwa anakata kona kuelekea kushoto wakati dereva wa gari aina ya Nissan alikuwa anaonesha ishara ya kuelekea kulia, lakini kwa bahati mbaya badala ya kulekea kulia alinyooka na barabara na kulifikia gari la Kim K na kusababisha magari hayo kukwaruzana.
Imeelezwa kuwa wawili hao waliendesha hadi Beverly Hills Hotelambapo walizungumza na kuyamaliza na kila mmoja akaendelea na safari yake bila polisi kuhusika.

No comments:

Post a Comment