aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Tuesday, March 18, 2014

RUBANI FARIQ ABDUL HAMID ASEMEKANA KUITOROSHA NDEGE YA MALAYSIA AIRLINES


Kamera za usalama zikimwonyesha rubani wa ndege ya Malaysia aina ya Boeing 777, Zaharie Ahmed Shah,  kwenye uwanja wa Kuala Lumpur.
Michoro inayoonyesha njia ambayo ndege hiyo huenda ilipitia kwenda kusikojulikana.
Mwanafunzi, Firman Siregar, akiwa na wazazi wake, ni mmoja wa abiria 239 waliokuwa katika  ndege hiyo yenye orodha ya safari namba  Flight MH370.
Rubani Zaharie Ahmad Shah.
Nyendo za ndege hizo zinavyokisiwa na wataalam.
Mwandishi wa habari akichukua picha nyumba ya  rubani Fariq Abdul Hamid eneo la Shah Alam, karibu na Kuala Lumpur.
Maafisa nchini Malaysia wamefichua kwamba wanadhani rubani mwenza katika ndege ya Malaysia iliyotoweka ndiye aliyezungumza maneno ya mwisho kabla ndege hiyo kutoweka.
Maneno hayo bado hayajabainika lakini yanasikika kama -- all right, augoodnight -- ''Kila kitu ki shwari au muwe na usiku mwema'', kabla ya vifaa vinavyowezesha ndege kutambulika katika mtambo wa rader kuzimwa.
Wachunguzi wanaangalia uwezekano kuwa huenda marubani walihusika katika tukio hilo.
Juhudi za kimatifa za kutafuta ndege hiyo pia zinazingatia njia mbili ambazo huenda ndege hiyo ilifuata kwani inaaminika kuwa ilipaa kwa saa kadhaa baada ya mitambo ya mawasiliano kuzimwa.
CHANZO: PICHA DAILYMAIL / HABARI BBC SWAHILI