aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Tuesday, March 25, 2014

HII NDIO PICHA YA MTOTO ALIE NA RISASI KICHWANI BAADA YA SHAMBULIO MOMBASA.. JITIHADA ZINAENDELEA KUOKOA MAISHA YA HUYU!! SOMA ZAIDI HAPA!!

Screen Shot 2014-03-25 at 11.02.10 AM Satrin Osinya ambae bado anarisasi kichwani mpaka sasa kutokana na shambulizi lililofanywa kanisani Mombasa na watu wasiofahamika Jumapili iliyopita ambapo mama yake mzazi aliuwawa.
Huyu aliembeba akiwa na huzuni inayoambatana na machozi ni Moses Gift katika hospitali ya Coast General, Mombasa ambapo picha ya Xray imeonyesha huyo mtoto bado ana risasi kichwani.
Imefahamika kwamba risasi iliyomuingia kichwani mtoto huyu ndiyo iliyomuua mama yake, yani baada ya kunyooshewa silaha mama alikua ana mkinga mwanae ndio risasi ikamuua yeye kisha ikaenda kutua kichwani kwa mwanae.
Madaktari wamekuwa wakitazama picha za Xray na Scan kuchunguza iwapo upasuaji utafanikisha kutolewa kwa risasi kichwani mwa Santrin bila kumpa maumivu au kuhatarisha maisha yake.
Santrin amekuwa akilia kwa uchungu alio nao kila wakati hospitalini huku babake akitizama tu ashindwe la kufanya huku machozi ya kakake Moses Gift mwenye umri wa miaka 13 yakiwaleta Wakenya kwenye taswira ya unyama waliofanya magaidi wasiojali hata watoto.
Madaktari Mombasa wamekuwa wakijadili uwezekano wa kumsafirisha Santrin hadi jiji la Nairobi kwa matibabu zaidi.