aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Tuesday, March 25, 2014

IDADI YA WATU WALIOPOTEZA MAISHA KATIKA MAPOROMOKO MAREKANI YAFIKIA 14

Waokoaji wakitafuta watu waliopotea katika maporomoko.
MAOFISA wa utawala katika jimbo la Washington nchini Marekani, wamepata miili sita zaidi baada ya maporomoko ya ardhi yaliyotokea siku ya Jumamosi.
Hii imefikisha idadi ya watu waliofariki kutokana na maporomoko hayo hadi 14.
Watu 176 bado hawajapatikana baada ya ukuta wa matope wenye urefu wa futi 177 kuporomoka karibu na mji wa Oso, Kaskazini mwa Seattle.
Zoezi la uokoaji bado linaendelea kwa kutumia helikopta na miale ya Laser, japo maofisa wanakiri kuwa wana matumaini madogo sana ya kupata majeruhi katika tukio hilo..
Rais Barack Obama ametangaza hali ya hatari katika jimbo hilo na kuwaamuru maofisa wote wa serikali ya jimbo hilo kushirikiana kutoa msaada wa dharura.
Gavana wa jimbo hilo ameitaja hali kuwa mbaya na ambayo haikutarajiwa.
Watu 176 bado hawajapatikana.
Jamaa na marafiki pamoja na wafanyakazi wa kujitolea, wanatumia misumeno na mikono mitupu kuondoa vifusi ili kutafuta wale waliopotea.
CHANZO: BBCSWAHILI