aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, March 29, 2014

PICHA ZINATISHAAAA..!! TAZAMA PICHA ZA VIBAKA WALIYOCHOMWA MOTO BAADA YA KUTUMIWA KUIBA COMPUTER..!!

Watu wawili ambao hawajafahamika majina yao wameuwawa kwa kuchomwa moto  na wananchi wanaozaniwa kuwa na hasira kali  katika kijiji cha Kagongwa wilayani Kahama  Mkoani Shinyanga baada ya kudaiwa kuiba  vitu mbalimbali ikiwemo Komputa.
Tukio hilo limetokea leo  majira ya saa tano asubuhi baada ya watuhumiwa hao kujaribu kuwakimbia viongozi wa Sungusungu waliokuwa wanawashikilia baada ya kuwakamata.
Kwa mujibu wa Mashuhuda wamesema vijana hao walikuwa ni tishio katika mji huo kutokana na kuiba marakwamara hivyo wananchi baada ya kuwakamata wameamua kuwachoma moto kwa madai kuwa iwe ni fundisho kwa  wengine.Wamesema Awali watuhumiwa walikamatwa na sungusungu ya kijiji cha Iponya wilayani humo Kabla ya kuamriwa wakaoneshe vitu hivyo ndipo wakapata mwanya wa kukimbia.Diwani wa kata ya Kagongwa Hamis Kashantole Ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa kata hiyo amekataa kuzungumzia tukio hilo kwa madai kwamba  hana muda wa kuongea.Jeshi la polisi wilayani Kahama limethibitisha kutoikea kwa tukio hilo na hadi sasa  uchungizi Unaendelea .

No comments:

Post a Comment