aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Tuesday, March 18, 2014

MILEY CYRUS AUMIZA KINYWA CHAKE KWA TATTOO MPYA ALIYOCHORA KWENYE LIPSI.


clip_image002Duh! Kweli kuishi kwingi ni kuona mengi, Dunia inaelekea mrama kutokana na vihoja vinavyoendelea kutokea kila kukicha hiyo inakuja kufuatia  Mwanamuziki wa kibao cha Wrecking Ball mwendawazimu ‘Miley Cyrus’ kuja na kioja cha aina yake baada ya kuamua kuumiza lipsi zake na kujichora tattoo ya rangi kwa kimombo colorful tattoo’   na kisha kutupia picha hiyo mtandaoni iliyoambatana  na ujumbe uliosomeka   “#sadkitty #f–kyeahtulsa,” Cyrus, 21”..
Miley Cyrus tattooPichani ni Miley Cyrus akionyesha Tattoo yake mpya aliyoichora kwenye Lipsi zake iliyo na picha ya mtoto wa paka ‘Kitty
Tangu kuanza kwa ziara yake ya muziki iliyopewa jina la BANGERZ, Miley amekuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wake   hasa kutokana na mfululizo wa vituko anavyokuwa akivifanya pindi anapokuwa jukwaani,  mojawapo ya tukio lililovuta vichwa vingi vya habari na kuandikwa sana  mitandaoni  ni kitendo chake cha  kukutanisha ndimi na mwanamuziki ‘Katty Perry’ alipokuwa akiperform katika ukumbi waStaples Center Los Angels mwezi uliopita.