aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Sunday, March 2, 2014

PNC AFUNGUKA UKWELI, NI KUTOKANA NA ALICHOFANYIWA NA OSTAZ JUMA NAMUSOMA..CHEKI HAPA 
Baada ya kile kilichoitwa ni unyanyasaji na udhalilishwaji wa msanii PNC na meneja wake Ostaz Juma Namusoma, wasanii wenzake pamoja na wadau mbalimbali wa muziki wamelaani sana kitendo cha meneja huyo kumdhalilisha msanii wake kiasi kile.

Wengi tumekuwa tukiona picha mtandaoni baada ya Ostaz Juma Namusoma kuziweka katika ukurasa wake wa faceboo. Lakini hatujajua ni nini kilichotokea kati ya watu hawa na kufikia kuwa ni story kubwa sana ya wiki hii..

Millardayo alifanya mahojiano na PNC na hiki ndicho alichokizungumza PNC Mwenyewe

"Kuomba samahani hiki kitu sijaona kama ni kitu kibaya kwangu hata kupiga goti kumuomba samahani- kwa sababu hata baba yangu siku zote nilipokuwa nikimkosea yaani ilikua kawaida yangu,baba bana nisamehe yaani kwa kwa upande wetu ni heshima tu nimechukulia’
"Kwa sababu  mwenyewe anadai yeye hajazijichapisha yeye zile picha,tulikuwa wengi kifupi sijajua siwezi kumlaumu nikasema ostaz umechapisha inshu zangu, kikubwa kuhusu haya mambo mi napotezea naangalia mambo yangu"
"Unajua ostaz wanamchukulia kama kaka yangu wakinipigia simu ndugu zangu wananilaumu wewe umemfanya nini ostaz,tumeshaongea na ostaz kinachofuata sasa hivi ni kuingia studio na kufanya kazi zangu kama kawaida".

Baada ya muhusika mwenyewe kuzungumza, Je wewe una maoni gani? 
By BongoToday