aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Tuesday, March 4, 2014

Kundi la Weusi Lamsimamisha LORD EYEZ baada ya kushutumiwa kwa wizi wa LAPTOP

Msemaji kampuni ya Weusi, Nick wa Pili amesema kuwa rapper Lord Eyez amesimamishwa na kampuni hiyo kutokana na kuvunja maadili.
 
Nick wa Pili amesema baada ya kupokea taarifa za Lord Eyez kushikiliwa na polisi huko Arusha kwa wizi wa Laptop walikaa kikao na kuamua kumsimamisha.
 
“Kitu ambacho naweza kusema kutoka Weusi ni kwamba Lord Eyez tumemsimamisha kazi kikampuni,” 

 “Uamuzi wa kumsimamisha tumeufikia jana na leo ndio tumeamua kutangaza rasmi kwamba Lord Eyez tumemsimamisha kazi na amesimamishwa kutokana na misingi na makubaliano ya kampuni,kulingana na maadili ya kampuni yetu na mawazo yetu kwa pamoja ndio yamefanya tukamsimamisha. Kwahiyo ni kwamba tumemsimamisha kutokana na makubaliano ambayo yalifikiwa ndani ya kampuni ambayo mengine yatabakia ndani ya kampuni.” Nikki wa Pili 
 
Uamuzi huo wa Weusi umekuja kufuatia taarifa kuwa Lord Eyez alikamatwa na polisi kwa tuhuma za wizi wa laptop Jumamosi, huko Arusha na baadhi ya picha za tukio hilo kuonekana. Taarifa hizo zimedai kuwa anatuhumiwa kwa wizi wa laptop aina ya ‘Dell’.
 
Mwaka juzi, Lord Eyez alikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za wizi wa Power Window za gari la Ommy Dimpoz, lakini Ommy alitangaza kumsamehe msanii huyo.