aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Sunday, March 2, 2014

BUNGE LA KATIBA NI UTALII..WAPO WALIO KUJA NA FAMILIA ZAO NA MA MADEREVA

Katika uchangiaji wa  masuala mbalimbali baadhi ya wajumbe hao wamekosa aibu kabisa. Wamediriki kuwasha vipaza sauti tena wakati wenzao au mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo, Ameir Panju Kificho  akizungumza,  na kupaza sauti wakitaka kupewa karatasi za kusaini ili kulipwa posho. Hicho ndicho kilichowapeleka Dodoma kweli?

Wajumbe hawa wamesahau kabisa kuwa Bunge hilo ni la kihistoria na nchi yetu haijawahi kuwa na bunge kama hili tangu tupate uhuru 1961.

Ukiacha wapenda posho, wapo wanaoibuka asubuhi na kusaini kisha kuingia mtaani na kuwaona tena ni mpaka mchana au jioni.  Hawana habari kabisa na kinachoendelea wao kikubwa ni posho tu.

Siku ambayo Rais Jakaya Kikwete alitangaza majina ya wajumbe 201, wapo wananchi walioponda uteuzi huo, lakini binafsi nilijua kipimo cha walioteuliwa kwa Watanzania ni hoja watakazokuwa wakitoa katika vikao vya bunge hilo.

Nilijua wazi kuwa hata wale wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wale wa Baraza la Wawakilishi, wataweka uzalendo mbele na kuacha masilahi ya vyama wanavyotoka.

Lakini imekuwa tofauti. Baadhi ya wajumbe hao wamedhihirisha kuwa wapo mjini Dodoma kwa ajili ya kulamba posho na kutetea masilahi ya vyama vyao vya siasa.

Wengi wamesahau kuwa wamechaguliwa na kuteuliwa kwa ajili ya kuwawakilisha Watanzania milioni 43 ndani ya Bunge hilo.

Baadhi yao badala ya kujadili masuala ya msingi wamekomalia nyongeza ya posho kwa madai kuwa wanayolipwa sasa ya Sh300,000 kwa siku, ni kiduchu na haitoshi kwa sababu gharama za maisha mjini Dodoma zimepanda.

Wanapendekeza kulipwa Sh500,000

Lakini nyumba za kulala wageni hapa Dodoma zinapangishwa kwa kati ya Sh20,000 hadi 80,000, chakula cha kawaida Sh6,000, kukodi teksi ni kati ya Sh3,000 hadi 6,000 sasa nyongeza hiyo ya posho ni kwa ajili ya nini?

Wapo waliokuja na familia zao, ndugu na jamaa, madereva na mambo chungu mzima. Huo msafara wa kazi gani?

No comments:

Post a Comment