aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, May 23, 2014

TAARIFA KWA UMMA KULAANI KITENDO CHA KUMFICHA MTOTO NASRA (4) CHUMBANI NA KUMFUNGIA NDANI YA KASHA KWA MUDA WA MIAKA MINNE ENEO LA KIWANJA CHA NDEGE, MANISPAA YA MOROGORO

nembo 3_thumb[1]
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto inalaani vikali tukio la ukatili na udhalilishaji dhidi ya mtoto Nasra (4) mkazi wa mjini Morogoro ambaye alifichwa chumbani ilhali amefungiwa ndani ya kasha na mama yake mkubwa kwa muda wa miaka nne, baada ya mtoto huyo kufiwa na mama yake mzazi.Kitendo hicho ni ukiukwaji wa haki za mtoto. Wizara inasisitiza kwamba mzazi au mlezi yeyote anayekubali jukumu la kulea mtoto anaowajibu wa kuhakikisha kuwa anampatia mahitaji yote muhimu ya kumwezesha mtoto kukua hadi kufikia utimilifu wake. Wizara inakemea vikali kitendo hicho na vingine vingi vya aina hiyo ambavyo vinaendelea kufanyika katika familia zetu na jamii kwa ujumla.Wizara inaziomba mamlaka zinazohusika na udhibiti wa vitendo vya ukatili dhidi ya watoto kuhakikisha kuwa watuhumiwa wote wanafikishwa mbele ya vyombo vya sheria ili haki iweze kutendeka na kuwa fundisho kwa wanaoendeleza ukatili dhidi ya watoto. Jamii inahimizwa kubadilika na kuhakikisha kuwa familia ambayo ndio kitovu cha jamii panakuwa ni mahala salama; na kuwahakikishia watoto haki zao za msingi  ikiwemo haki ya kuishi, kulindwa, kuendelezwa, kushiriki na kutobaguliwa.

Wizara inapongeza Uongozi wa Manispaa ya Morogoro hasa Afisa Ustawi wa Jamii, Jeshi la Polisi kupitia Dawati la Jinsia na Watoto  na Afisa Mtendaji wa Kata ya Kiwanja cha Ndege kwa kufuatilia suala hili kwa karibu. Vile vile, Wizara inapongeza majirani na vyombo vya habari kwa uzalendo wao mkubwa wa kufichua ukatili aliofanyiwa mtoto huyu maana taarifa zao zimesaidia kunusuru uhai na maisha ya mtoto Nasra.
Wizara inamwelekeza Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Morogoro awasiliane na Afisa Ustawi wa Jamii husika kuona uwezekano wa kumkabidhi mtoto Nasra kwenye taasisi zinazohusika na matunzo ya watoto ili awe kwenye mikono salama, wakati taratibu za kisheria zikifanyika dhidi ya wanaohusika na ukatili huo.
    Anna T. Maembe  
 KATIBU MKUU
                                                                  
23 Mei, 2014