aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, May 8, 2014

PICHA 10 ZA MAHABUSU WALIOVUA NGUO NA KUNG'ANG'ANIA MLINGOTI WA BENDERA YA TAIFA KUSHINIKIZA KESI ZAO KUSIKILIZWA HARAKA

Inspector Henry akiwasihi mahabusu hao wawili wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji, kuachia mlingoti wa Bendera ya Taifa na kurudi kwenye chumba cha mahakama kwaajiri ya taratibu za kesi.

Matukio ya ajabu yanayofanywa na mahabusu wanaoshinikiza kesi zao kusikilizwa haraka ikiwa ni mbinu wanazoamini zitasaidia katika kile wanachoeleza kuwa ni kudai haki zao yanaendelea kuonekana ambapo jana mahabusu jijini Mwanza walifanya tukio la aina yake. 
 
Mahabusu wawili kati ya sita wanaoshikiliwa kwa tuhuma za mauaji jana walijaribu kutoroka kutoka kwenye mstari wa utaratibu wa kuingia mahakamani na kisha kung’ang’ania mlingoti wa bendera ya Taifa huku mmoja wao akivua nguo zote na kubaki mtupu.
 
Tukio hilo lilitokea majira ya saa nne asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Nyamagana, jijini Mwanza.
 
Thobias Warioba, mmoja kati ya mahabusu hao ndiye aliyevua nguo zote na kubaki mtupu na kisha kupiga kelele akiwa ameshikilia mlingoti akieleza kilio chake.
 
“Haiwezekani tangu mwaka 2011 tulipokamatwa hadi sasa kesi zetu hazijasikilizwa. Wengine tumebambikiwa kesi. 

"Tunaomba haki zetu, polisi wanatuonea, vyombo vya habari tunaomba mtusaidie tumekaa muda mrefu bila kusikilizwa na hatujui hatma yetu tangu mwaka 2011tulipokamatwa.


"Tumechoka kukaa mahabusu, tunaomba kesi zetu zisikilizwe.” Alisema Thobias Warioba.
 
Inspector wa polisi alijitambulisha kwa jina la Henry aliwataka watuhumiwa hao waondoke katika mlingoti na kuvaa nguo ili waingie mahakamani kwani kitendo walichokuwa wakikkifanya ni kosa la jinai..
 
“Pamoja na maamuzi yenu haya, lakini mtambue mnavunja sheria na hili ni kosa jingine la jinai, hivyo ni vyema mkaondoka kwenye mlingoti huu na kuingia mahakamani. Malalamiko yenu tumeyasikia na yatashughulikiwa.”Alisema Inspecta Henry.
 
 Askari polisi wakiwalinda mahabusu wawili kati ya sita wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji
 Inspector Henry (shati la bahari) akiwa na Inspector Veda (mwenye koti) wakisikiliza hoja za Thobiasi Warioba (35), aliyeamua kuvua nguo zote na kubaki mtupu akiwa ameng’ang’ania mlingoti wa Bendera ya Taifa
 Ushawishi ukiendelea
 Mahabusu Thobiasi Warioba (aliye mtupu) pamoja na mwenzake Hamis Ramadhani katu katu waking’ang’ania mlingoti wa bendera ya Taifa huku wakishinikiza kuzungumza na waandishi wa Habari.
 Baada ya kuzungumza na waandishi wa habari mahabusu hao walikubali kurejea chumba cha Mahakama.

 Mashuhuda nao hawakuwa mbali kushuhudia tukio hilo..yaaani nishiidaah
 
Nae mmoja wa maafisa wa mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza ambaye hakutaka jina lake litajwe, alieleza kuwa ushahidi wa kesi za watuhumiwa hao bado haujakamilika na kwamba kesi zao haziwezi kusikilizwa na mahakama ya Wilaya kwani haina uwezo, na badala yake zitaendelea kutajwa tu kisha zitahamishiwa Mahakama Kuu.

No comments:

Post a Comment