aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, May 23, 2014

DALILI ZA TATIZO LA KUTOPATA UJAUZITO

IKIWA ni rahisi au vigumu kujigundua kama unauwezo wa kupata ujauzito au la, au kwa mwanaume kama ana uwezo wa kumpa mwanamke mimba au la. 
Tatizo la kutofanikiwa kupata ujauzito kwa mwanamke  linahusiana moja kwa moja na kuwepo na tatizo kwa mwanaume.
Unaweza kusema kama una tatizo hili endapo unaishi katika mahusiano ya kutafuta ujauzito kwa zaidi ya mwaka mmoja lakini hakuna mafanikio.
Ili mwanamke apate mimba ni lazima awe na sifa za kupata ujauzito, na ili mwanaume aweze kumpa mwanamke mimba ni lazima  awe na sifa za kumpa mwanamke mimba.
Matatizo haya yapo kwa pande zote mbili.
Wakati wa kutafuta ujauzito, ni vema mwanamke na mwanaume washirikiane kwani mwanaume unaweza kujiona huna tatizo kumbe ukija kupima mbengu zako utajikuta unatatizo kubwa.
Matatizo kwa mwanamke
Mwanamke mwenye tatizo la kutopata ujauzito anaweza kuwa na mojawapo ya matatizo haya yafuatayo;
Atakuwa amekaa na mume au yupo katika mahusiano ya kutafuta mtoto kwa zaidi ya mwaka lakini hakuna mafanikio, hulalamika maumivu ya chini ya tumbo mara kwa mara au yanaweza yasiwepo, maumivu ya hedhi, kuvurugika mzunguko na kutoona ute wa uzazi.
Wengine hawana hamu ya tendo la ndoa au kutojihisi raha wakati wa tendo, maumivu wakati wa tendo au kutokwa na uchafu ukeni wakati mwingine huambatana na muwasho na harufu.
Anakuwa na historia aidha ya kutumia njia za uzazi wa mpango, kuharibu au kutoa mimba, historia ya kuzaa, au kufanyiwa upasuaji wa aidha uzazi au mirija. Ingawa wengine hawana  historia hizi.
Nini cha kufanya?
Endapo utahisi una matatizo ya kutopata ujauzito na unazodalili kama hizo hapo juu au huna, basi ni vizuri umuone daktari wa magonjwa ya matatizo ya uzazi katika hospitali za mikoa. Uchunguzi utafanyika kuangalia mfumo wako wa homoni au vichocheo vya uzazi, vipimo vya kizazi na mirija na vingine ambavyo daktari atashauri.
Uchunguzi na matibabu huchukua muda mrefu, ni vema kufuatilia  kwa makini.
Athari kubwa zinazotokea mara nyingi katika uzazi kwa mwanamke ni kuziba kwa mirija ya mayai.
Mvurugiko wa mfumo wa homoni, matatizo ndani ya kizazi ambayo yanaweza kuwa uvimbe au maambukizi.
Uwezekano wa kutibiwa na kufanikiwa upo endapo utazingatia.
Matatizo ya uzazi kwa mwanaume
Mwanaume kama atazingatia uchunguzi na tiba naye anaweza kufanikiwa ingawa akigundulika kama anatatizo tiba yake huchukua muda mrefu.
Uchunguzi wa mwanaume ni kuangalia mbegu za uzazi na kupima korodani.
Mwanaume unaweza kujifahamu kama unatatizo endapo utakuwa na dalili zifuatazo; siyo lazima zote lakini mojawapo, upungufu wa nguvu za kiume,
kuishi na mwanamke zaidi ya mwaka mmoja lakini hakuna mimba, kutoa manii nyepesi sana na zenye harufu mbaya, manii nyepesi hutoka mara moja ukeni unapomaliza tu tendo la ndoa.
Maumivu ya muda mrefu ya korodani, maumivu ya kiuno, maambukizi ya mkojo ya mara kwa mara, uvutaji wa sigara kwa muda mrefu, unywaji wa pombe kali, na matumizi ya madawa ya kulevya mfano bangi na mirungi na mengineyo.
Nini cha kufanya?
Matatizo haya hutibika kwa daktari wa matatizo ya uzazi kwenye hospitali za  mikoa. Vipimo vya mbegu za uzazi vitafanyika kuangalia kiwango cha mbegu na ubora wake kama zina uwezo wa kutungisha mimba.
Vipimo vingine itategemea na uwepo wa matatizo mengine ya uzazi kwa mwanaume kama kuwahi kumaliza tendo la ndoa, kushindwa kufanya tendo la ndoa, upungufu  wa nguvu za kiume, uchovu mkali baada ya tendo la ndoa, maumivu ya  kiuno, korodani na maumivu ya njia ya mkojo.
Wahi hospitali kwa uchunguzi na tiba.

No comments:

Post a Comment