aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, May 30, 2014

MSANII NYOTA NDOGO APATA AIBU YA MWAKA, ACHUNGULIWA UCHI WAKE LIVE ..AISHIA KUMWAGA MACHOZI......

 
Msanii  maarufu  wa  Kenya, Nyota  Ndogo  amejikuta  akimwaga  machozi  kutokana  na  aibu  aliyoipata  baada  ya  kundi  kubwa  la  watu  kumshuhudia  akiwa  uchi  wa  mnyama  huku  akijipaka  mafuta  pasi  yeye  kujua..... 


Nyota  Ndogo  alikumbwa  na  dhahama  hiyo  alipokuwa  aki perform  katika  show  moja  nchini  Kenya  hivi  karibuni. Kwa  mujibu  wa  maelezo  ya  msanii  huyo  aliyoyatoa  katika  ukurasa  wake  wa  facebook  ni  kuwa, akiwa  katika  Show  hiyo, mwenyeji  wake  alimpatia  chumba  kwa  ajili  ya  kubadili  nguo, akaingia  na  kuvua  nguo  zote  na  kisha  kuanza  kujipamba. Amekuja  kustuka  kuwa  anachunguliwa  na  watu  baada  ya  kusogolea  kioo  kilichokuwa  ndani  ya  chumba  hicho  ambapo  aliwaona watu  hao  wakimwangalia.... 
"Yani nimekwenda show.nikapewa chumba chakubadili nguo.nimevua nguo zote najipaka mafuta pole pole kumbe najiangalia kwa kioo kumbe upande wapili naoneka kila kitu.yani nimekosa amani...aibu nilio iona mungu ndio anajua.sijui wamechukua video..haya ngoja tusubiri," amendika  kwa  uchungu  msanii  huyo


Msanii  huyo  amemtwisha  zigo  la  lawama  mwenyeji  wake  aliyempatia  chumba  hicho  ili  hali  akijua  kinaonekana  kwa  nje 
"Hapana nilibakisha cha ndani na nyonyo ilikua na nguo pia.kitu sielewi ni alienipeleka kubadili nguo ina maana hakujua nje naonekana?maana aliambia kioo hiki jiangalie mpaka miguu."Ameandika  Nyota  Ndogo  na  kuongeza 
"Kuajulisha tu ili kama walichukua video mukiiona mujue niliwataarifu" 

 
Aidha, Nyota  Ndogo  aliutumia  pia  ukurasa  huo kuwasihi  watu  hao  wasitoe  picha  zake  za  uchi  au  video  kama  walirekodi ili  kumtunzia  heshima  mbele  ya  watoto  wake


"Wafikirie wanangu," Ameandika  msanii  huyo.