aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Tuesday, May 27, 2014

MAJI YA KUPONYA MAGONJWA GUMZO,WANANCHI WAMIMINIKA KUYAOGA..WENYE VIRUSI,MAGONJWA SUGU WASHANGILIA

WANADAMU wanazidi kuegemea kwenye imani utata! Hivi karibuni, watu mbalimbali wenye magonjwa wamekuwa wakimiminika nchini Nigeria na kuoga maji ya bwawa yanayodaiwa yanaponya magonjwa papo hapo. 
Watu mbalimbali wenye magonjwa  wakimiminika kwenye maji ya bwawa nchini Nigeria na kuoga  wakiwa na imani ya kuponywa magonjwa yao.
Watu hao wakiwemo wazee, vijana waume kwa wake na wenye magonjwa mbalimbali wamekuwa wakizama kwenye maji hayo kwa urefu wa futi tatu hadi nne, wengi wakiwa uchi au nguo za ndani tu.
Wengine huchota maji hayo na kuosha sehemu yenye tatizo hasa wale wenye kushindwa kuona au wenye vidonda sugu kama vile kansa, Ukimwi nakadhalika.
Bwawa hilo limepewa jina la Orimiri lipo umbali wa kilomita 3 kutoka mji wa Nachi, Enugu nchini humo na liligunduliwa na watu wa Kabila la Fulani.
Umati wa watu ukizidi kujitosa kwenye maji hayo huku wengi wao wakiwa utupu.
Tangu kugunduliwa kwa bwawa hilo, zaidi ya watu 3000 wameshafika kuyaoga maji hayo kuanzia asubuhi hadi saa 12 jioni.
Hata hivyo, hakuna taarifa za moja kwa moja na uwazi kwamba watu wamepokea uponyaji.
Nigeria ni nchi yenye matukio mengi ya kiimani licha ya mambo ya kisiasa ambapo mpaka sasa wananchi wake wamekuwa wakikumbana nayo.
Wananchi wakiwa wamejaa bwawani kama kwa Babu wa Samunge.
Baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakiwaambia waumini wao kuamini zaidi katika uponyaji wa Mungu.
Nchini Tanzania, miaka ya karibuni aliibuka Mchungaji Ambilikile Masapile ‘Babu wa Samunge’ akidai ana maji ambayo mtu mgonjwa akinywa anapata uponyaji.
Watanzania wengi, wakiwemo viongozi wa serikali walimiminika kwenye Kijiji cha Samunge, Loliondo kunywa kikombe chenye maji hayo lakini baadaye ilikuja kubainika kwamba, hakukuwa na uponyaji wowote zaidi ya kumwachia babu huyo utajiri.

No comments:

Post a Comment