aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Monday, May 5, 2014

HAKIKA WEMA SEPETU NAE ANASTAHIRI KUPEWA TUZO, ANGALIA LIST YA WANAUME MASTAR ALIOKULA NAO URODA(NA MAREHEMU AKIWEMO) AVUNJA REKODI TANZANIA NZIMA

Wema Sepetu ni miongoni mwa wasanii wenye mvuto sana hapa Tanzania na tunaweza kusema hata Afrika Mashariki. Amejipatia umaarufu mara ya kwanza baada ya kushinda taji la Miss Tanzania mwaka 2006. Baada ya hapo alianza kumake headlines kwa skendo za mapenzi kabla hajaingia rasmi kwenye tasnia ya filamu, na aliyemuingiza alikuwa ni Marehemu Steven Kanumba. Kwa kipindi hiki kisichozidi miaka 10 ya umaarufu wake amefanukiwa kufanya mambo makubwa katika tasnia ya filamu kwani ameonesha kipaji cha hali ya juu sana. Licha ya hayo umaarufu wake unakuzwa zaidi na skendo za hapa na pale na mara nyingi ni skendo za mapenzi. Leo tumeamua kuwaletea list ya wanaume aliotoka nao mpaka sasa kwa kipindi hiki cha miaka 8 ya umaarufu wake.

1. MR. BLUE
Mara baada ya kuwa Miss Tanzania mwaka 2006 Wema kama kawaida yake hakutaka kuwa na uhusiano na mtu asiyekuwa na jina mjini. Aliamua kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na mwanamziki huyu ambaye kwa kipindi hicho alikuwa ndio anatawala soko la mziki wa kizazi kipya. Hatujui waliachana vipi lakini hivi karibuni Mr. Blue alinukuliwa akisema kuwa Wema alimfilisi kipindi anatoka nae. Kama hukusoma hii habari ISOME HAPA 

2. T.I. D
Baada tu ya kuachana na Mr. Blue tulisikia tetesi kuwa anatoka na Msanii mwingine Khalid Mohamed almaarufu kama TID. Hatukujua mwisho wa uhusiano wao ulikuwaje lakini baada ya kuachana tulisikia TID ametoa wimbo ambao ulikuwa ni kama dongo kwa Wema, ulikuwa unaitwa NILIKATAA

3. STEVEN KANUMBA
Baada ya kuruka ruka huku na kule hatimaye Wema aliangukia kwa Aliyekuwa nguli wa tasnia ya filamu hapa Bongo Marehemu Steven Kanumba (RIP BROTHER). Mahusiano yao yalimake headline mjini lakini yaliisha vibaye kwani kila Mtanzania alijua baada ya Wema kuwekwa selo na Kanumba baada ya kumfanyia fujo. Japokuwa waliachana lakini Wema humshukuru Kanumba kila siku kwani ndiye aliyemuingiza katika tasnia ya filamu baada ya kugundua kuwa ana kipaji sana.

4. JUMBE
Huyu dogo dogo kwa kweli hakuwa maarufu lakini alikuwa na pesa, nahisi hicho ndicho kitu kilichomfanya Wema ahamiashie majeshi yake baada ya kutoka kwa KANUMBA

5. CHALZ BABA
Baada ya kutoka kwa Jumbe, Wema alihamishia majeshi kwa Mwanamuziki wa dansi Chalz Babaenzi hizo akiimbia bendi ya African Stars.

6. DIAMOND
Kutoka kwa Chalz BABA, Wema alihamishia mapenzi yake kwa mwanamuziki Diamond Platnumz. Kama kawaida yake alitazama ni nani anayeng'ara kwenye tasnia ya burudani bongo na akafankiwa kumtia himayani Diamond Platnumz enzi hizo Diamond ndio alikuwa msanii anayeng'ara zaidi baaada ya kutwaa tuzo tatu katika TUZO ZA KILI MUSIC AWARD. Mahusiano yao yalikuwa hot kiasi kwamba yaliweza kuzua gumzo katika mitandao ya kijamii kabla ya kuachana.

7. CLEMENT
Huyu jamaa alimnasa Wema mara tu baaada ya kuachana na Diamond, alitumia pesa alizokuwa nazo na Wema alianza kuonyesha jeuri ya pesa alizokuwa anapewa na CK. Alinunua nyumba ya Mil 400, akafungua Ofisi yenye thaman ya mil 85 na kubadilisha magari kama nguo. Mwisho wa mapenzi ya Wema na CK ulikuwa mbaya kwani Wema alipokonywa vitu vyake alivyokuwa amepewa na kuishiwa jeuri tena mjini.

8. DIAMOND TENA
Baada ya kuachana na CK aliamua kurudisha majeshi kwa Diamond ambapo mpaka sasa wako wote na wamekuwa wakimake headline kwenye social media kila siku. teenz Choice tunawatakia kila la kheri ili tunamuomba Wema atulie tu kama kweli hapo amependa aweke mizizi. Kila la KHERI DIAMOND NA WEMA
source:paparazzihuru