aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, May 9, 2014

WEMA ANASA USHAHIDI WA KAJALA KUMUIBIA BWANA

Unaweza ukaficha siri na ukaamini hakuna atakayejua bila kukumbuka kuwa hakuna siri ya watu wawili! Hatimaye Wema Isaac Sepetu amenasa ushahidi wa aliyekuwa rafikiye kipenzi, Kajala Masanja wa kumwibia aliyekuwa bwana’ke, Clement au CK, yule kigogo wa ikulu.
Wema Sepetu.
MIL. 13 KISINGIZIO TU
Habari za mjini kwa wiki nzima ni kusambaa kwa ujumbe mfupi (SMS) za kimapenzi za Kajala na CK ambazo sasa zimefunua kisa kamili cha mastaa hao kuhitilafiana huku Sh. Milioni 13 zikiwa kisingizio tu.
WEMA ALIKUWA ANATAFUTA USHAHIDI?
Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na mastaa hao, kupatikana kwa meseji hizo ni kama mpango wa Mungu, kwani sasa kitendawili kimeteguka.
Baadhi ya meseji zilizonaswa.
“Wema alikuwa anatafuta ushahidi kama kweli Kajala anatembea na CK hivyo sasa amepata ushahidi.
“Mwenye macho haambiwi tazama na kama hujui kusoma hata picha huoni? Ama kweli kikulacho ki nguoni mwako!” Kilisema chanzo hicho.
Habari za ndani zilieleza kuwa meseji hizo zilikutwa kwenye simu ya CK na mwanamke mwingine ambaye naye anadaiwa kutoka na kigogo huyo, aliyetajwa kwa jina moja la Naima aliyekwenda kumbwagia ‘zigo’ Wema kwa ajili ya ushahidi.
Kajala Masanja.
Ilisemekana kwamba Naima alimuomba simu CK kwa kuwa ya kwake ilikuwa mbovu.
Habari zilizidi kudai kuwa baada ya CK kumpa mpenzi wake huyo simu yake, kumbe zile meseji alizokuwa akichati na Kajala alikuwa amesahau kuzifuta ndipo zilipobambwa.
Mpashaji wetu aliweka wazi kwamba meseji zile zilimshangaza Naima kwa kuwa yeye alikuwa ni mmoja wa watu ambao walikuwa hawaamini kabisa kama kulikuwa na ukweli wowote kuhusu tuhuma za Kajala kutembea na CK.
NAIMA ACHANGANYIKIWA
“Yaani Naima alipoziona meseji alichanganyikiwa kabisa, alikuwa kama kachomwa sindano ya ganzi kwani alikuwa ni mmoja wa watu ambao  hawaamini kabisa kama kweli Kajala anatembea na CK.
“Naima alipokaa vizuri ndipo akaanzisha timbwili lenye ujazo mkubwa na CK,” kilisema chanzo hicho.
Mnyetishaji wetu aliendelea kutiririka kuwa katika SMS hizo ambazo zilionesha waziwazi namba ya Kajala, zilikuwa zikielezea namna CK alivyokuwa akimuomba msamaha Kajala kwa kutopokea simu yake.
Kajala na Wema wakati wa ushosti wao.
HUU HAPA MZIGO
Mtiririko na meseji hizo ulikuwa hivi;
CK: “Mama mimi sipendi kukatiwa simu  pze, ok sawa lakini mi nakupenda.
Kajala: Kwa hiyo ndiyo unaniambiaje?
CK: Umeamua kuniblock?
CK: Kwa nini hupokei simu zangu?
CK: Unaponikatia simu wakati mimi naongea sijapenda sijui nijielezeje mama haya sawa.
Kajala: Fanya mambo.
MZIGO MIKONONI MWA ‘MNYAMWEZI’ WEMA
Ilisemekana kwamba baada ya Naima kuona meseji hizo alizihifadhi ili akamfikishie Wema ‘Myamwezi’ na kumuonesha jinsi rafiki yake alivyokuwa siyo mwaminfu kwake kitu ambacho alikifanikisha.
Habari zilidai kuwa baada ya Wema kuona SMS hizo alipatwa na mshtuko mkubwa kwani alikuwa haamini kama ni jamboanaloweza kulifanya rafiki yake Kajala.

No comments:

Post a Comment