aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, May 30, 2014

FAHAMU UMRI SAHIHI WA MWANAUME KUOA NA MWANAMKE KUOLEWA


WAFUNGA NDOA WAWE WAMETIMIZA UMRI 
UNAOKUBALIKA KISHERIA: 
Mwanamke na mwanaume wawe 
wametimiza miaka 18 ili kufunga ndoa. 
Hata hivyo mwanamke anaweza kuolewa 
akiwa na umri wa chini ya miaka18 lakini 
sio chini ya miaka 15 kama atapata idhini 
ambayo hutolewa na baba na kama hayupo 
ni mama au kama wote wamefariki idhini 
itatolewa na mlezi wa binti huyo. 
Kama wote wamefariki basi hatahitaji 
idhini. Kuna wakati katika mazingira fulani 
mahakama inaweza kutoa idhini kwa binti 
kuolewa akiwa na miaka 14 lakini si chini 
ya hapa ikiwa ataonekana kwa mfano ana 
mimba. Pia mwanaume anaweza 
kuruhusiwa na mahakama kuoa akiwa na 
umri wa miaka chini ya 18 lakini lakini si 
chini ya 16 kama ataonyesha kuelewa 
jukumu lake kama mtu mzima. Lakini hii ni 
pale ambapo kuna tatizo kama la kumpa 
msichana mimba ndipo mahakama inaweza 
ikatoa idhini. Katika ombi la kuoa la SHABIRI 
A. M. VIRJI (1971) HCD NO. 407 la Mahakama 
Kuu ya Tanzania, mwombaji alikuwa na 
miaka 16 lakini alimpa mimba binti wa 
miaka 18. Mahakama katika kuchunguza 
ombi la mvulana la kuoa ilitoa kibali kwa 
sababu wote wawili walipendana sana na 
wazazi wao hawakuwa na kipingamizi cha 
wao kuoana. 
MFUNGISHAJI NDOA KUTOKUWA NA 
MAMLAKA: 
Kama wanaofunga ndoa wanajua wazi 
kuwa anayewafungisha ndoa hana 
mamlaka hayo na kwa makusudu 
wakakubali awafungishe ndoa basi ndoa 
hiyo itakuwa ni batili. Mfungishaji ndoa ili 
kuwa na mamlaka anapaswa kusajiliwa na 
Msajili Mkuu wa Ndoa na kupewa leseni ya 
kufungisha ndoa.

No comments:

Post a Comment