aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, May 17, 2014

Mrema ashauri Polisi wapewe asilimia 10 ya Mali wanayokamata ili iwe kichocheo cha kufanya kazi kwa bidii

 
Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Augustine Mrema (MB, Vunjo, TLP) amependekeza askari polisi wapewe asilimia 10 ya thamani ya mali wanayokamata ili iwe kichocheo cha kufanya kazi kwa bidii na kuacha kuomba na kupokea rushwa. 

Pia, alishauri askari kuongezewa posho kutoka shilingi 5,000 ya sasa mpaka 7,500/= kwa sababu fedha hiyo ya awali, haiwezi kuwafanya askari kujikimu katika mahitaji ya kila siku.

Huku akisifu utendaji wa jeshi la polisi, Mrema ameshauri askari wawe wanapewa motisha kwa lengo la kuwapa morali ya kufanya kazi zaidi ya ilivyo sasa. 

Alisema kwa kufanya hiyo kutasaidia kupungua kwa vitendo vya uhalifu nchini kwani hali hiyo itawaongezea askari moyo wa kufanya kazi.

No comments:

Post a Comment