aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, May 31, 2014

ANGALIA PICHA ZA MAREHEMU GEORGE TYSON MASAA 4 KABLA YA KIFO CHAKE PAMOJA NA GARI ALILOPATA NALO AJALI.

IMG_4162
Marehemu Geogre Tyson pichani hapa alikuwa yupo kijiji cha Chilonwa Chamwino kwenye utoaji wa madawati katika shule ya msingi Chaula iliyopo Dodoma.

 Baada ya kumaliza shughuli hii huku akiwa kama producer wa The Mboni Show mauti yalimkuta majira ya saa 12 jioni masaa 4 tu toka tuanze safari ya kurudi Dar es Salaam maeneo fulani hivi kama unataka kukaribia GAIRO mjini.
Katika gari hilo walikuwa watu 8 ila yeye pekee ndio aliyepoteza maisha na wengine kupata majiraha mwilini pamoja na dereva wa gari hilo. Kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa Morogoro katika  hospital ya mkoa Morogoro, baadae asubuhi mwili utaanza safari ya kuelekea Dar es Salaam.
IMG_4166IMG_4176 IMG_4213IMG_4214IMG_4215
Kweli ajuae mwisho wetu ni Mungu pekee. Tunaishi kama vile tunajua maisha yetu yataisha lini kumbe tunajidanganya. Haya matukio yote ni kwa ajili yetu kuamka na kujifunza kitu. Tumrudieni Mungu, tuungame dhambi zetu maana hakuna ajuae siku wala saa yake itakuwa lini. R.I.P Tyson na wote mliotutangulia.

No comments:

Post a Comment