aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, May 30, 2014

MTOTO ALIYEFUNGIWA KWENYE BOKSI KWA SASA ANAPUMULIA MASHINE MUHIMBILI

 
MTOTO Nasra Rashid (4) aliyefichwa katika boksi kwa miaka minne mkoani Morogoro, sasa anaopumulia mashine  katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Nasra, alilazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alipohamishiwa Mei 26 mwaka huu kwa ajili ya uchunguzi zaidi akitokea katika Hospitali ya mkoa wa Morogoro.


Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Daktari bingwa wa Magonjwa ya Watoto, David Kombo, aliyekuwa zamu alisema Nasra, aliwekewa mashine maalum ili kusaidia kupata hewa ya Oksijeni baada ya kuanza kupumua kwa shida.


Alibainisha kuwa hali ya mtoto huyo ilikuwa ikiendelea vizuri lakini juzi usiku ilibadilika na hivyo kuwekewa mashine ya kupumulia.


Dk. Kombo alisema kutokana na hali hiyo, madaktari wa zamu juzi waliamua kumfanyia vipimo na kubaini anasumbuliwa na Ugonjwa wa Nemonia.


Dk. Kombo, alisema mtoto huyo akipata nafuu ya ugonjwa wa Nemonia, ataendelea na vipimo vikubwa vya mwili mzima ikiwamo moyo na figo.


Alisema licha ya ya kumpatia dawa za Nemonia, wanaendelea kumpatia chakula na dawa baada ya vipimo vya awali kubaini ana Utapiamlo.


Ofisa Muuguzi wa zamu, Iluminata Sokani, alisema licha ya kupumulia mashine hali ya mtoto huyo inaendelea kuimarika kila wanapomfanyia vipimo kujua maendeleo yake.


Naye mama mlezi wa Nasra, Josephine Joel alisema kabla ya mtoto hajawekewa mashine ya kumsaidia kupumua, alimuambia anaumia kifuani na kiunoni


Mtoto Nasra alifichuliwa na Mei 2, mwaka huu na majirani ambao walimweleza Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kiwanja cha Ndege Dia Zongo kuwa alikuwa amefichwa katika boksi na Mwanamke aliyetambuliwa kwa jina la Mariamu Said mkazi wa Kata hiyo mkoani Morogoro.


Majirani hao walimweleza Zongo kuwa Nasra alifichwa ndani ya boksi tangu akiwa na umri wa miezi tisa 2009 na kwamba hafanyiwi usafi wala kumtoa nje.

No comments:

Post a Comment