Katika hali ya kawaida kufanya mapenzi kuna faida nyingi, lakini
linapokuja suala la kuzidi kiasi tunapata matatizo ya msingi ambayo
huleta madhara kwa watu wanaoendekeza sana ngono.Kuna watu ambao
hawezi kulala bilakufanya mapenzi na huku wengine wakikosa uwezo wa
kuvumilia hata kwa siku mbili au tatu.Mtu anaweza kuwa na mke na
kujikuta kila siku anatumia 'chakula cha usiku' kwa sababu tu hakuna
wa kumkataza na kwamba ana haki ya kufanya hivyo kwa sababu amelipa
mahari.Hilo linaweza kuwa jambo jema kwaupande mwingine, lakini
uchunguzi unaonyesha kuwa watu wengi kati ya watu wanaolalamika
kupoteza hisia za kimapenzi hutoka katika kundi la watu wapenda
ngono.Pamoja na tatizo hilo, yapo madharamengine mengi ambayo mtu
asiyekuwa na kiasi katika tendo la ndoa anaweza kukabiliana nayo,
hivyo ni vema tukajifunza ili tusiwe watu wa kuendekeza miili kiasi
cha kulazimika kufanya mapenzi kila tunapokutana hata kwenye nguzo ya
umeme na chini ya miti kwa vile tu miili imetaka kufurahika.Twende
pamoja katika kutazama madhara hayo kwa kina.KUPOTEZA HAMU YA
TENDO.Watu wenye pupa za kufanya mapenzi hupoteza haraka hisia za
kimapenzi kwa wapenzi wao kutokana na sababu za kisaikolojia
zinazoweza kujitokeza wakati wa ufanyaji wa tendo la ndoa mara kwa
mara.Sababu hizo zinaweza kuwa ni pamoja na zile za kumzoea
mwenzakiasi cha kukosa msisimko hata anapomuona akiwa mtupu.Aidha
kukinai haraka staili za kimapenzi kunatajwa kujitokeza kutokana na
kukutana mara kwa mara kwa aina zile zile za mapenzi na pengine sehemu
moja, kitanda kimoja na chumba kile kile, jambo ambalo linaweza
kumfanya mhusika asione jipya kutoka kwa mwenza wake na hivyo kupoteza
hamu naye na kuhisi kama hawezi tena kushiriki tendo la ndoa
kikamilifu.KUUJAZA MWILI TAMAA KUBWA.Tabia ya kufanya mapenzi mara
kwamara huongeza uzalishaji wa homoni mwilini na kuufanya mwili uwe na
msukumo mkubwa wa kutaka kuridhishwa kwa tendo la ndoa bila kukosa na
hivyo kumfanyamhusika asiwe mtu mwenye uwezo wa kuzuia tamaa na kukosa
chaguo la nani wa kufanya naye mapenzi nakwa wakati gani?Watu
wanaojiendekeza katika kufanya mapenzi mara kwa mara ndiyo wale ambao
kila wanayemtazama barabarani humtamani bila kujali hadhi yake.Hawa
ndiyo wanaobaka, kusaliti ndoa zao hata kwa watumishi wa ndani au
kufanya mapenzi na watoto wao wa kuwazaa kwa vile akili zao huwa
zimeathirika kwa tamaa ya mapenzi.Unapokuwa mtu wa kufanya mapenzi
mara kwa mara huwezi kuwa na uwezo wa kuzuia tamaa yako. Mumeo
akiondoka siku mbili unatamani kuwa hata na houseboy ili akukate kiu
ya penzi.KUPOTEZA RAHA KAMILI YA TENDO.Raha ya tendo hutegemea sana
hisia iliyokuzwa kutokana na mapenzi sahihi na kiu ya kufanya mapenzi,
hivyo basi ukiwa mtu wa kufanya mapenzi kila mara unawezakupoteza
msisimko wa tendo na kujikuta unapata furaha ambayo haikutoshi
kumaliza tamaa yako.Kama ni mapenzi utakuwa unayafanya kwa mazoea tu
na msisimko wako utakuwa mdogo!KUPOTEZA NGUVU ZA MWILI.Madhara mengine
yanayoweza kupatikana kwa kufanya mapenzi mara kwa mara ni pamoja na
kupoteza nguvu nyingi za mwili.Kama tujuavyo tendo la ndoa hasa kwa
wanaume huwafanya watumie nguvu nyingi, hivyo kuufanya mwili uchoke.
Aidha lishe inapokuwa ndogo kwa wafanya mapenzi mwili hukosa nguvu za
kutosha kuhimili misukosuko ya kimaisha.Sambamba na hilo mbegu za
uzazi zinazotoka kwa wanaume wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa
dhaifu.KUPATA MAGONJWA.Kama tulivyojifunza kuwa watu wanaofanya
mapenzi mara kwa mara huwa na tamaa na hujikuta wanafanya mapenzi
holela ambayo huweza kuwasababishia magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi,
lakini ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na msukumo wa kutosha hasa kwa
wanawake huwafanya waishiwe msisimko na kuzifanya sehemu zao za siri
kutotoa ute unaoweza kuwakinga na michubuko wakati wakujamiiana na
hivyo kuwasababishia michubuko itakayoweza kuleta maambukizi ya haraka
ya magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi.
No comments:
Post a Comment