aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, May 23, 2014

MAFUFU AUGUA, ASHINDWA KUMZIKA KUAMBIANA

STAA wa filamu za Kibongo, Jimmy Mafufu licha ya kutoa suti ya shilingi 400,000 aliyozikiwa nayo marehemu Kuambiana, alishindwa kumzika rafiki yake huyo kipenzi baada ya kuugua ghafla siku ya mazishi na kulazwa hospitali. 
Muigizaji wa filamu za Kibongo, Jimmy Mafufu.
Akizungumza na Ijumaa, Mafufu alisema kuwa alijikuta akipatwa na maumivu makali pamoja na homa hali iliyosababisha alazwe katika Hospitali ya Mico iliyopo Kinondoni Makaburini, Dar.
“Ukweli tumeondokewa na jembe tena mtu mwenye akili sana na mwenye elimu, sijui tasnia itakuwaje, nimeumia kushindwa kumzika lakini nashukuru nilijitoa kwa hali na mali,” alisema Mafufu.