aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, May 30, 2014

KUFANYA MAPENZI OFISINI HUVURUGA SAIKOLOJIA YA MTU.

Kula nanasi kunahitaji nafasi, wengi wamekuwa wakishawishika 
kufanyamapenzi katika eneo la kazi kutokana na kupendana ama 
vishawishi mbali mbali kutoka kwa kinadada hususani katika mavazi. 
Sina maana mbaya ninaposema kina dada kwasababu wengi wao ndio 
wanaoacha sehemu zao nyeti wazi, kwamfano kuvaa nguo fupi sana na 
kuvaa vitop vinavyoonyesha sehemu kubwa ya maziwa wazi.Kwa asilimia 
miamoja watu wengi wanaofanya mapenzi kwa kuiba katika maeneo kama ya 
ofisini huwahawakumbuki kuvaa kinga kutokanana mihemumko mikali na ya 
haraka kuliko kawaida wanayokuwa nayo kwa wakati huo. Ni vyema 
kujihadhali ma mihemuko hii kwani madhara yake ni makubwa.Mihemuko hii 
huwakumba watu wote hata ambao wako katika ndoa, kutokana na 
vishawishi vya mwenzake basi anajikuta amezama katika saa za kazi. 
Tabia hii ikifanyika mara tatu huanza kuwa kama sehemu ya majukumu ya 
wezihawa wa mapenzi. Kinadada wanaovaa nguo fupi katika makazi ya watu 
huenda wakawa wanafanya hivyo kwasababu ya fasheni, wengine kutafuta 
mvuto kwa wafanyakazi wenzie, lakini kwa wanaume huwa ni kishawishi 
kimoja kikubwa sana.Kumbuka unapaswa kuishinda faragha yako na 
kujitambua kuwa hupaswi kufanya mapenzi na mke wa mtu au mume wa mtu. 
Unapoona vishawishi kama hivi jaribu kuwa bize na kazi, chukulia poa 
tu japokuwa wadada wengi huwa na njia mbali mbali za kukufanya ukanasa 
kirahisi kwa mfano kama mnakumbuka skendo ya Monica Lewinsky na 
aliyekuwa rais wa Marekani wakati huo walichokifanya ofisini na baadae 
kuja kuwa ni skendo kubwa sana.Hasara ya mapenzi hayo ya kiwizi wizi 
katika masaa ya kazi ni kupata maambukizi ya Ukimwi bila kufahamu 
kwani utakuwa umemzoea mfanyakazi mwenzio kwa jinsi alivyo smati 
katika kazi, hivyo hutafikilia kama anawatu wengine nje ya kazi. Pia 
kuna maambukizi ya magonjwa ya zinaa, ambayo kwa wanawake hujificha 
kwa muda kabla ya kuonekana haraka kama wanaume.