aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, May 31, 2014

JOHARI AMTUPIA CHUCHU VIJEMBE MSIBANI

STAA wa Bongowood, Blandina Chagula ‘Johari’ anadaiwa kumtupia vijembe kiaina msanii mwenzake, Chuchu Hans ambaye ‘anabanjuka kimalovee’ na mkurugenzi mwenza wa Kampuni ya RJ, Vincent Kigosi ‘Ray The Greatest’. 
Staa wa Bongowood, Blandina Chagula ‘Johari’.
Tukio hilo lilichukua nafasi kwenye msiba wa mwigizaji Sheila Haule ‘Recho’ Sinza-Palestina, Dar, hivi karibuni ambapo vijembe viliibuka baada Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Nyerere’ kumuuliza kwa lugha ya utani Chuchu kuwa RJ itachangia nini msibani hapo, Johari akadakia:
“Kampuni yangu si ya uchochoroni au ya chumbani, nina TIN namba kabisa siyo kama hiyo nyingine, iweje umuulize asiyehusika...”
Baada ya Johari kutamka maneno hayo, waombolezaji waliokuwepo msibani hapo walipigwa na butwaa na kuhoji kulikoni?
Mastaa wa Bongo Muvi akiwemo Chuchu Hans (wa pili kushoto) wakiwa msibani kwa Recho.
Johari amekuwa akidaiwa kuwa na uhusiano na Ray kipindi cha nyuma huku kukiwa na taarifa kuwa Chuchu ana kampuni iitwayo Chura ikimaanisha Chuchu na Ray hivyo ilitafsiriwa kuwa alikuwa akiipiga kijembe kwa madai kuwa haiwezi kufikia levo za RJ.
Alipofuatwa na paparazi ili kupata ufafanuzi juu ya ishu hiyo, Johari hakuwa tayari kwani alisema ana majonzi ya kuondokewa na kipenzi chake Recho hivyo hakutaka malumbano na watu katika kipindi hiki kigumu.