aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, May 24, 2014

ROSE NDAUKA AELEZA ALIVYOWAMWAGA WANAUME NA KUTULIA NA MALIKI

KAMA kawa, leo katika Exclusive Interview Mwigizaji maarufu wa filamu za kibongo Rose Ndauka akiwa na mumewe Malikitunaye mwigizaji Rose Ndauka ambaye anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni.Kwenye maisha yake ya sanaa, amepitia mambo mengi ambayo yanasisimua, katika makala haya utayapata kwa ukamilifu wake:


ALIVYOANZA KUIGIZA
Ilikuwa ni mwaka 2007, Dairekta na muigizaji wa filamu nchini, Single Mtambalike ‘Rich’ alimshawishi Rose Ndauka aingie kwenye tasnia ya sanaa.
Kama bahati, Rose alikuwa akienda kumtembelea rafiki yake katika Kundi la Kamanda ambalo Rich alikuwa akiigiza, ndipo akashawishiwa kujiunga na sanaa.
Rich, wasanii wenzake akiwemo Baba Haji, JB, alipomuona kwa mara ya kwanza aligundua kabisa kuwa Rose anaweza kuigiza ila alikuwa hajajitambui, hivyo baada ya kuoneshwa njia, fasta akaitumia fursa.
ALIPENDA KUTAZAMA FILAMU
Licha ya kutowahi kuigiza lakini Rose alipenda sana filamu za Kifilipino pamoja na tamthilia mbalimbali za Kizungu zilizokuwa zikiendelea kwenye runinga mbalimbali.
paparazi: Nje ya Rich kukuonesha njia, ujasiri zaidi wa kuendelea na uigizaji uliupata wapi?
Rose Ndauka: Baba Haji ndiyo alisisitiza kuwa naweza, alinipa ushawishi mkubwa, akaniambia nisikate tamaa, kweli nikajitahidi na mpaka leo hii napasua anga za uigizaji hadi kufikia hatua ya kupewa tuzo mbalimbali, namshukuru Mungu.
paparazi: Baada ya kuingia kwenye kundi la akina Rich, ilisemekana kuwa mlivuka mipaka na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na ndiyo maana ulikuwa na nafasi kubwa ya kucheza filamu, unalizungumziaje hilo?
Rose Nda
ka: Mh! Siwezi kusema kuwa ni kweli kwa sababu mimi ninachojua Rich alikuwa ni bosi wangu na mpaka leo namuheshimu kama bosi.
Rose Ndauka akiwa na mwanae
paparazi: Wakumbushe wasomaji wa paparazi Jumamosi filamu yako ya kwanza kabisa kuigiza.
Rose: Ilikuwa inaitwa Swahiba, nilicheza kama Aisha msichana aliyekuwa akisoma chuo.
paparazi: Tukitoka kwenye upande wa filamu na uigizaji, maisha ya kawaida kwako wewe kama msichana umewahi kuwa na uhusiano na wanaume tofauti na wengine waliripotiwa katika vyombo vya habari je, ni kwa nini uliamua kuwabwaga na kuhamia kwa baba mtoto wako (Maliki Bandawe) unaweza kusema?
Rose Ndauka: Niligundua kuwa hawakuwa na ‘future’ na mimi hivyo nikaachana nao, nikaamua kutulia na Maliki ambaye ndiye anayetarajia kunioa soon.
paparazi: Baba mtoto wako mlikutana wapi na una uhakika gani kama ana future na wewe?
Rose Ndauka: Mwanaume mwenye future utamjua tu, kwa huyu naamini nimefika, nilikutana naye Tanga tulikuwa tunafahamiana kabla ya kupendana na kilichotuweka karibu ni kazi hivyo, alivyorusha nanga nikaamua kumkubalia.
paparazi: Wewe ni staa unayependwa na wengi, unazungumziaje usumbufu kutoka kwa wanaume wakware? Baba mtoto wako anaipokeaje hali hiyo?
Rose: Niliwahi kusumbuliwa na wengi kabla sijaingia kwenye uhusiano kamili, kuna niliowahi kuwakubalia lakini kuna niliowakataa kwa sababu hawakuwa na vigezo, baada ya kuwa mama, najiheshimu na baba mtoto wangu ananiamini anachonikumbisha ni ‘ku-take care’ tu.
paparazi: Kuna habari zilitufikia wakati bado hamjapata mtoto na Maliki kuwa uliwahi kupigana klabu kwa kugombea penzi la njemba wa nje ya nchi, unalizungumziaje hili?
Rose: Mh! Siyo kweli, kwanza mimi starehe za klabu nilifanya sana nilipokuwa na umri wa miaka 19-21 baada ya hapo mtu akikwambia aliniona klabu atakuwa anakudanganya, sijakanyaga huko muda mrefu sana.
paparazi: Katika maisha yako umewahi kumfumania umpendaye?
Rose: Nimewahi kumfumania mpenzi (siyo Maliki) mara  mbili lakini nilichoshukuru ni kwamba sikuwahi kuachwa katika fumanizi, anayeachwa mara nyingi ni yule ninayemkuta na mpenzi wangu.
paparazi: Je, umewahi kumfumania baba mtoto wako? Ikitokea je utafanyaje?
Rose: Siombi itokee lakini ikishatokea ndiyo nitajua nifanyeje ila watu wasitegemee kama nikimfumania nitamuacha, nitafanya uchunguzi nitakapobaini sababu za kufanya hivyo, nitachukua uamuzi sahihi.
paparazi: Umewahi kupata skendo za kutembea na wapenzi wa rafiki zako akiwemo huyu baba mtoto wako, unalizungumziaje hilo?Rose: Sijawahi na hata baba mtoto wangu hajawahi kuwa na uhusiano na rafiki yangu yeyote kabla.

credit:gpl