KUNA baadhi ya sababu zinazosababisha watu kuoana pasipo kufanya
maamuzi sahihi. Wanandoa wengi huingia katika ndoa wakitegemea mambo
mengi kubadilika, kitu ambacho ni makosa yanayosababisha ndoa nyingi
kuvunjika.Kabla ya kuoa/kuolewa unapaswaUjitambue Kwanzana ujiulize
maswali kadhaa, kwanza jiulize;(1)Je huu ni wakati sahihi?(2)Kwa
ninimtu huyu? na(3)Unamuoa au kuolewa na mtu atakaye kuwa sambamba na
malengo yako katika maisha yako yote?Wakati kuna sababu kadhaa za
kumuoa/kuolewa na mtu sahihi, pia upande mwingine kuna sababu kibao
zinazopelekea watu kuoa watu wasio sahihi kwao. Kabla ya kusema
"Ndiyo" zingatia sababu tano hapa chini zinazokufanya uoe au kuolewa
na mtu ambaye si sahihiambae baadae hupelekea kutengana na kupeana
taraka.(1) Tumekuwa katika mahusiano kwa muda mrefu. Kuwa katika
mahusiano kwa kipindi kirefu sio sababu pekee ya kufanikiwa kumpata
mwenye mafanikio katika maisha yako, unaweza ukawa umemvumilia kwa
muda mrefu na sasa ukaamua tu kwasababu umekwisha zoea tabia yake na
kufuata usemi wa"maji ukisha yavulia nguo shartiuyaoge".(2)Msukumo wa
Marafiki- Rafiki zangu wote wamekwisha OA/KUOLEWA....... itabidi na
mimi nioe/niolewe. Kufuata mkumbo wa makundi katika jamii sii kitu
kizuri, kwani ndoa siyokitu cha kubeep na kuacha. Jipange kwanza na
muda ukifika basi itaingia katika ndoa yenye mpangilio mzuri wa
maisha.(3) Sidhani kama nitaweza.Usipo jiamini na kujipenda mwenyewe
sidhani kama itakuwa rahisi kumpenda mtu mwingine unayetegemea kuwa
nae maishani.(4) Mategemeo ya kuboresha tabia ya mwenza wako. Tukisha
oana nitambadilisha tabia. Cheti cha ndoa siyo leseni ya kumrazimisha
mwenzi wako kubadilika kwa lazima. Jaribu kuwa na subira na kumtafuta
mwenzi mnae endana nae kitabia.(5)PESA- Anakazi nzuri naamini ataleta
pesa au anatoka katika familia ya kitajiri. Kunaukweli mkubwa katika
misemo ya wahengayani "kama ukiowa kwaajili ya pesa, basi utazilipa"
japokuwa kuwa na pesa sio vibaya, lakini hii haitazuia pia haizuii
kuwa na muunganiko mbaya wa ndoa.Wanandoa wengi huingia katika dimbwi
hili ambapo wengine hushinikizwa kuoa kulingana na taratibu za kimila
au kidini. Lakini pia wazazi wakati mwingine huchangia ndoa nyingi
kuvunjika, ikiwa ni kwa kuwachagulia wananandoa mke au mume.Vijana
ambao bado hamjaoa au kuolewa"Jitambueni Kwanza", fikirini kwa kina
kabla ya kufanya maamuzi yasiyo sahihi ambayo yatawagharimu muda wenu
na kupata mateso ya muda mrefu.
No comments:
Post a Comment