aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Tuesday, February 11, 2014

“Nataka Mwanaume Mchakalikaji, anaezijua mishemishe za mjini na sio Goigoi”….Amanda

AMANDA Poshi mwigizaji wa filamu Bongoamesema kuwa kwa sasa yupo single hana mchumba wala mume bali anasubiri atokee mwanaume mwenye sifa ambazo kaziweka wazi, endapo atatokea mtu wa namna hiyo atajikwalia ushindi kwa kumpata yeye na kuwa mke wa maisha yake.
“Nahitaji mwanaume mchakalikaji, mishemishe za mjini anazijua, anijali na kunipenda zaidi sipo tayari kuolewa na mwanaume asiyejielewa, mtu mwelewa ambaye hauwezi kupishana Kiswahili na kuzua balaa la ugomvi siwezi bab,”anasema Amanda.
Moja ya masharti yake mengine ni pamoja na mwanaume ambaye atakuwa tayari kumuoa awe tayari kumruhusu kuendelea na kazi ya uigizaji asimzuie kwani itakuwa ndio sababu ya kutengena kwao, mtu ambaye atakuwa tayari kwa hayo atampatia zawadi ya kumzalia watoto wawili kwa maisha yao.
Amanda Poshi