aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, February 15, 2014

HII NI AIBU:MREMBO ANASWA KWA WIZI WA CHUPI ZA WAGONJWA HOSPITALI..TAZAMA PICHA ZA MATUKIO HAPA

MREMBO Asna Elias mkazi wa maeneo ya Manzese mkoani hapa, ameingia matatani baada ya kutiwa mbaroni kwa wizi wa nguo za ndani za mgonjwa aliyelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
Asna Elias akiwa mikononi mwa polisi baada ya kunaswa kwa wizi wa nguo za ndani.
Tukio hilo la aina yake, lilitokea Jumatatu iliyopita mchana wa jua kali nyumbani kwa Kigogo wa UWT kupitia CCM, Bi. Mwajuma Malingo anayeishi Mtaa wa Holowera Kata ya Mji Mpya.
Asna akiziba uso wake kwa aibu baada ya kunaswa kwa wizi.
Akizungumza na paparazi wetu kuhusu ishu hiyo, Malingo alisema kwamba akiwa anaoga alisikia sauti ya vishindo vya mtu aliyekuwa akitembea.
Polisi akiangilia baadhi ya nguo za ndani alizokamatwa nazo Asna.
Kiongozi huyo wa UWT, alisema baada mtu huyo kusimama aliamua kumchungulia kupitia tundu la funguo ndipo alimuona Asna akianua nguo za ndani na nyingine ambazo zilikuwa mbichi na kuzisunda kwenye pochi na mfuko wa rambo.
Asna akiwa chini ya ulinzi.
“Kama unavyoonaniko na khanga moja tu, nilikuwa bafuni naoga  nikasikia vishindo, nilipochungulia kwenye tundu la funguo nikamuona huyu msichana anaanua nguo za mgonjwa aliyelazwa Hospitali ya Mkoa ambazo nimetoka kuzifua sasa hivi, nikajifunga khanga na kutoka nje na kuanza kumfukuza huku nikimwitia mwizi, cha ajabu na yeye alipaza sauti kwamba hakuwa mwizi bali alinifumania na mume wake,” alisema Malingo.
 
Asna akiwa na aibu baada ya tukio hilo.
Malingo aliongeza kuwa, kufuatia mayowe ya mwizi aliyotoa, watu walijitokeza na kuanza kumpa kichapo msichana huyo huku wengine wakitaka kumchoma moto.
Wakati dada huyo akiendelea kula kichapo alitokea paparazi wetu aliyewapigia simu askari wa kike waliokuwa doria ambao walifika na kumtia mbaroni msichana huyo.
Asna akipewa vidonge vyao.
Askari hao walimpeleka  Kituo Kidogo cha Polisi Kata ya Mji Mpya akafunguliwa jalada la kesi namba MJ MPY/RB/18/2014 WIZI kisha kupelekwa mahabusu ya kituo kikuu.
Asna akishushwa kituo cha polisi.
Aidha, Bi. Malingo alisema kwamba hivi karibuni amekuwa akiandamwa na vibaka nyumbani kwake kwani wiki kadhaa zilizopita wezi walivunja dirisha la chumba cha kijana wake Ally na kuiba redio ya ya shilingi 800,000, deki ya 200,000 na simu ya shilingi 100,000.